Brittany Murphy mwigizaji na mwimbaji kutoka nchini Marekani


Brittany Murphy at the London premiere of Happy Feet, November 26, 2006

Brittany Anne Murphy-Monjack alifariki tarehe 20 Desemba mwaka 2009 akiwa na umri wa miaka 32

alikuwa mwigizaji na mwimbaji kutoka nchini Marekani.

Alipata kuonekana katika filamu kama vile Clueless, Girl, Interrupted, 8 Mile, Uptown Girls, Sin City, Happy Feet, na Riding in Cars with Boys

Amepata kuigiza kwa sauti katika filamu ya Luanne Platter ya katuni kwa ajili ya mfululizo wa TV ya King of the Hill.

Filamu ya Luanne Platter ya katuni iliyoigizaBrittany Murphy kwa sauti

Filamu yake ya mwisho iliitwa Abandoned, ambayo ilitegemewa kutolewa mwanzoni mwa mwaka wa 2010.

Wazazi wake, Sharon Kathleen Murphy na Angelo Bertolotti, walitalikiana akiwa na umri wa miaka miwili,

na Murphy akalelewa na mama'ke huko mjini Edison, New Jersey, na baadaye mjini Los Angeles, walipohamia.

kwa hiyo Murphy aliweza kujiendeleza zaidi katika kazi zake za uigizaji

Murphy wakati wa uhai wake aliwahi kusema kwamba mama'ke hakuwahi kujaribu kuzuia shughuli zake, na anamhesabu mama'ke kama ndiyo chachu ya mafanikio yake ya baadaye

"Pale nilipomwomba mama'ngu tuamie mjini California, aliuza kila kitu na kuhamia kule kwa ajili yangu.......Siku zote huniamini.

Brittany Murphy Alilelewa katika familia ya wa Baptist na baadaye wakaja kubadili na kuwa kwenye dhehebu la taasisi fulani ya Kikristo ambayo si jumuia katika taasisi za Kikristo zingine

www.mzunguko.com


Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu