Je wajua mwandishi wa kwanza muafrika aliyeandika kazi zake kwa lugha ya kiingereza na lugha ya Gikuyu

December 21, 2018

Ngugi wa Thiongo amezaliwa tarehe 5 januari 1938 ni mwandishi mkenya aliyeandika kazi zake kwa lugha ya kiingerza

lakini siku hizi anatumia lugha ya Gikukuyu

 

Maandishi yake ni pamoja na riwaya,tamthilia,hekaya,insha na uhakiki.

 

Ameanzisha gazeti la lugha ya Gikuyu Mũtiiri.

 Tangu mwaka 1982 ameishi nje ya Kenya akifundisha kwenye vyuo vikuu mbalimbali kama , New York na Irvine/California

 Ngugi amezaliwa Kenya katika kijiji cha Kamiriithu karibu na Limuru, wilaya ya Kiambu katika jamii ya Wagikuyu 

akabatizwa James Ngugi.

 

Alikuwa mtoto wa tano wa mke wa tatu wa baba yake Thiong'o wa Nducu

Baba  yake alikuwa mkulima aliyepoteza shamba lake kutokana na Waingereza kuteka na kutwaa Nyanda za Juu za Kenya

 

James alisoma shule za wamisionari za Kamaandura (Limuru), Karinga (Mangu) na Alliance High School (Kikuyu). Katika miaka ile akawa Mkristo.

 

Wakati akisomashule familia yake iliathiriwa na vita ya Maumau ikawa kaka yake aliuawa na mama yake aliteswa

 Baada ya kumaliza Alliance High akasoma Makerere akahitimu kupata digrii ya Kiingereza mwaka 1963.

 

Akafunga ndoa na Nyambura mwaka 1961 akazaa naye watoto sita katika miaka iliyofuata.

 

Mwaka 1962 aliandika tamthilia yake ya kwanza "The Black Hermit". Baada ya digrii alirudi Nairobi alipofanya kazi ya uandishi wa gazeti 

RIWAYA YA KWANZA

Mwaka 1964 akachukua nafasi ya masomo huko Chuo Kikuu cha Leeds. Hapo Uingereza alitunga riwaya ya "WEEP NOT, CHILD"

(1964) akiwa mwandishi wa kwanza kutoka Afrika ya Mashariki aliyetunga riwaya kwa Kiingereza.

 

Alisimulia hadithi ya kijana Njoroge mwenye ndoto ya kuendeleza elimu yake lakini anakwama kati ya ndoto zake na hali halisi ya maisha ya Kiafrika chini ya ukoloni

Aliendelea kwa "THE RIVER BETWEEN" (1965) akichora picha ya kijiji kilichopasuliwa kati ya wakristo na wafuasi wa dini ya asili.

 Mwaka 1967 alitumia historia ya vita ya Maumau na maarifa ya familia yake kwa ajili ya riwaya ya "A GRAIN OF WHEAT".

 

Ngugi ameendelea kutumia Gikuyu pekee kwa ajili ya riwaya lakini amefundisha na kutunga insha kwa Kiingereza.

 

Kati ya maandiko yaliyofuata ni "Detained" (Daiari ya gerezani - 1981); "Decolonizing the Mind: The Politics of Language in African Literature" (Kuondoa ukoloni rohoni -

 

siasa ya lugha katika fasihi ya Afrika 1986) alimodai waandishi Waafrika watumie lugha zao za kienyeji badala la lugha za Kiulaya; Matigari (1987) alimotumia hadithi ya kiutamaduni wa Gikuyu

 Mwaka 2004 Ngugi alirudi mara ya kwanza Kenya lakini alipata maarifa mabaya akishambuliwa na wahuni na kuibiwa mali na mke wake akibakwa.

 

Shabaha muhimu wa ziara yake ilikuwa kutangaza riwaya yake mpya kwa Gikuyu "Muroogi wa Kigogo".

 

Kiini cha imani ya Ngugi ni ya kwamba kwa kutumia lugha za kienyeji pekee waandishi waafrika watafikia wanachi wa kawaida na kushinda ukoloni mamboleo rohoni.

 Tatizo alilo nalo hapo ni ya kwamba lugha za kienyeji zinarudi nyuma haraka katika mazingira ya kisasa hata zikiendelea kuzungumzwa na kusikilizwa kwa redio si lazima  kwa sababu zinasomwa pia.

 

www.mzunguko.com

 

 

 

 

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon