Jeshi la Zimbabwe lalaumiwa kwa 'kutumia nguvu kupita kiasi' katika makabiliano na wafuasi wa upinzani

December 19, 2018

 

 

Jeshi la Zimbabwe lilitumia "nguvu nyingi" dhidi ya waandamanaji wa upinzani baada ya uchaguzi wa kiti cha Urais.

 

Hayo yamesemwa na tume maalum iliyoundwa kuchunguza kiini cha ghasia zilizotokea nchini humo.

 Watu 6 waliuwawa, baada ya vikosi vya jeshi kutumwa ili kukabiliana na waandamanaji hao waliozua ghasia katika maeneo kadhaa ya mji mkuu Harare mnamo Agosti 1.

 Tume huru ya uchunguzi , inasema jeshi lilitenda mabaya makubwa bila huruma, wakati ilipoamua kuwamiminia risasi waandamanaji waliokuwa wakitoroka.

 Lakini baadhi ya viongozi wa upinzani wanalaumiwa kwa kuchochea ghasia

 Wanajeshi na polisi walikabiliana na waandamanaji ambao walimiminika barabarani, baada ya kuibuka madai kwamba chama tawala cha Zanu-PF, kiliiba kura Julai 30.

 

Ripoti hiyo inasema Matokeo ya uchunguzi yanabaini kuwa mauaji ya watu hao 6, yalitokana na hatua ya jeshi na polisi," 

 

"Matumizi ya risasi yaliyoelekezewa watu, hasa walipokuwa wakitoroka, yanaonyesha bayana kuwa hayakuidhinishwa hasa kutokana na ukubwa wake," inaongeza ripoti hiyo

 Tume hiyo iliyo na wanachama 7 na ambayo iliundwa na Rais Emmerson Mnangagwa, kufuatia ushindi wake finyu wa Urais, ilibaini kuwa kutumwa kwa jeshi kutuliza uhasama huo mjini Harare ulifanywa kwa kufuata sheria.

 Mwenyekiti wa tume hiyo ni rais wa zamani wa Afrika Kusini Kgalema Motlanthe na aliyekuwa Mkuu wa Majeshi wa Tanzania Jenerali Davis Mwamunyange ni miongoni mwa wajumbe wake.

 

Ripoti hiyo pia imekishutumu chama cha upinzani cha MDC Alliance, kwa kuchochea ghasia, hasa kutokana na hotuba ya baadhi ya viongozi wake.

 

"Ikiwa maandamano hayo hayangekabiliwa, hali hiyo ingeongezeka na kuwa vigumu kuthibitiwa na hatimaye kuwa mbaya zaidi" inasema  ripoti hiyo inasema.

 

www.mzunguko.com

 

 

 

 

 

 

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon