Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Adolf Hitler anajitangaza kuwa kiongozi wa ngazi ya juu katika jeshi la ujerumani mwaka 1941

December 19, 2018

Adolf Hitler alikuwa dikteta wa Ujerumani kuanzia mwaka 1933 hadi kifo chake

[tarehe 19 mwezi wa 12 mwaka 1941  Adolf Hitler anajitangaza  kuwa kiongozi wa juu katika jeshi la  ujerumani]

 

Alihutubia  kwa dharau na chuki ya kimbari dhidi ya watu wote wasio Wagermanik na hasa dhidi ya Wayahudi.

 

Alisababisha Vita Kuu ya Pili ya Dunia na mateso ya watu milioni kadhaa.

Hitler alivutiwa sana na mfano wa Benito Mussolini, kiongozi wa kifashisti wa Italia, aliyefaulu mwaka 1922 kupindua serikali ya Italia kwa maandamano makubwa ya wafuasi wake kuelekea Roma.

 Adolf Hitler (kulia) pamoja na dikteta wa Italia Benito Mussolini

 

Mwaka 1923 Hitler alijaribu kumwiga Mussolini kwa kupindua serikali ya jimbo la Bavaria - kama utangulizi wa kupindua serikali ya kitaifa huko Berlin - lakini alikamatwa na kuhukumiwa kwa uasi huo kifungo cha miaka mitano,

 ingawa alitumikia miezi tisa tu hatahivyo Chama chake kilipigwa marufuku

 

Akiwa gerezani aliandika kitabu kilichoitwa "Mein Kampf" ("Mapambano Yangu")

 alijaribu kueleza imani na siasa zake. katika kitabu  chake  alieleza pia chuki dhidi ya Wayahudi na itikadi yake ya ubaguzi wa kimbari

Katika itikadi hiyo aliwazungumzia  watu wa Ulaya ya Kaskazini aliowaita "Waaria", na wale ambao ni duni zaidi ni watu weusi

 

Maafisa wachache wa jeshi  la Ujerumani walipanga mara kadhaa kumwua Hitler. Tarehe 20 Julai 1944 alijeruhiwa na bomu ya Stauffenberg lakini hakufa

 Gazeti la Marekani "Stars and Stripes" la tarehe 2 Mei 1945 latangaza kifo cha Hitler.

 

Tangu Januari 1945 Hitler alikaa katika boma imara chini ya ardhi kwenye ikulu yake mjini Berlin. Hakutoka mjini tena

eneo ambalo Adolf hitler alijificha mpaka  kifo chake na  mke wake 

 

Tarehe 25 Aprili 1945 Berlin yote ilizungukwa kama kisiwa na jeshi la Wasovyeti 

na tangu 28 Aprili waliingia katika kitovu cha Berlin. Habari zilifika Berlin ya kwamba makamu wake Hitler kama Himmler na Goering walijaribu kutafuta mapatano na Marekani au Uingereza.

 

Hitler aliwatangaza ni wasaliti akaamuru kuwakamata lakini amri hizi hazikutekelezwa tena maana hawakuwa karibu naye.

 

Tarehe 30 Aprili aligawa sumu kwa wote waliokuwa pamoja naye katika boma chini ya ardhi akawaruhusu kuondoka;

 

aliagiza sumu ijaribishwe kwa mbwa wake mpendwa "Blondi". 

 

Mnamo saa 15.30 Eva Brau ambaye ni mke wake  alijiua kwa kumeza sumu na Hitler alijipiga risasi kichwani.

 

Wasaidizi wa mwisho walibeba maiti hadi bustani ya ikulu na kuziweka katika shimo kutokana na mlipuko wa bomu; hapo wakazichoma kwa petroli.

 

 

www.mzunguko.com

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload