Tetesi za Soka Ulaya Jumanne 18.12.2018: Isco, Guardiola Pogba, na Mourinho


Pep Guardiola

Kocha wa Manchester City Pep Guardiola anataka kumsaini kiungo mshambuliaji wa Real Madrid na timu ya taifa ya Uhispania Isco, 26, baada ya msimu kukamilika.

Tayari mazungumzo ya awali kati ya miamba hao wa England na mchezaji huyo yameshafanyika.

Manchester United itawapasa kutoa kitita cha pauni milioni 24 kama wataamua kumfuta kazi kocha wao Jose Mourinho kabla ya kufungwa kwa dirisha dogo la usajili la mwezi Januari

Kiungo wa zamani wa Liverpool Danny Murphy amesema muda wa kumfuta kazi Mourinho ni huu.

Danny Murphy

Wakuu wa ligi ya Premia wanataka kufanya mazungumzo na wachezaji weusi ili kutafuta njia bora za kupambana na ubaguzi mchezoni - wachezaji weusi wanatazamiwa kuvigomea vyombo vya habari kama sehemu ya mapambano dhidi ya ubaguzi

Klabu ya Chelsea inajipanga kuwafungia mashabiki wanaofanya ghasia nje ya uwanja wao wa Stamford Bridge kutohudhuria mechi za klabu hiyo.

Hivi majuzi, klabu hiyo imewafungia kwa muda kupisha uchunguzi mashabiki wake wanaodaiwa kumtolea shutuma za kibaguzi nyota wa Manchester City, Raheem Sterling.

Klabu ya Juventus imekutana na wakala Mino Raiola kuzungumzia uhamisho wa mchezaji nyota Paul Pogba wa Manchester United.

Pia mazungumzo hayo yamehusisha usajili wa mlinzi kinda wa Ajax Matthijs de Ligtmet mwenye miaka 19 na kuongeza mkataba wa mshambuliaji kinda wa Italia mwenye miaka 18 Moise Kean.

Vigogo hao wa Italia wanataka kumrejesha Pogba jijini Turin baada ya kubaini kuwa United wanataka kumuuza katika dirisha la usajili la mwezi Januari

www.mzunguko.com


Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu