Mwanasiasa dikteta kutoka Urusi aliye sababisha vifo vya mamilioni ya watu

Terehe 18 mwezi wa 12 mwaka 1878 alizaliwa Josef Stalin, dikteta wa Umoja wa Kisovyeti na aliyetawala urusi kuanzia mwaka wa (1924 hadi1953)

Joseph Vissarionovich Stalin

alikuwa mwanasiasa Mrusi kutoka Georgia aliyeshiriki pamoja na Lenin katika Mapinduzi ya Urusi ya 1917 na kuwa kiongozi wa chama cha kikomunisti halafu kiongozi mkuu wa Umoja wa Kisovyeti baada ya kifo cha Lenin.

Alitawala Urusi kama dikteta kwa unyama na kusababisha vifo vya mamilioni ya watu.

Alifaulu kujenga uchumi na jeshi la Umoja wa Kisovyeti na kutetea nchi dhidi ya mashambulio ya Ujerumani wakati wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia

Alikuwa kati ya washindi wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia akapanua utawala wake juu ya nchi za Ulaya ya Mashariki na ya Kati kama vile Poland, Uceki, Hungaria, Romania, Bulgaria na sehemu ya mashariki ya Ujerumani.

Stalin alikubaliwa kama kiongozi wa nchi zote za kikomunisti pamoja na China, Vietnam na Korea ya Kaskazini hadi kifo chake.

alifuatwa na Nikita Krushchov kama kiongozi wa chama na Umoja wa Kisovyeti

www.mzunguko.com


Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu