Raisi wa Urusi Vladimir Putin ataka muziki wa rap udhibitiwe na serikali

December 16, 2018

Rais wa Urusi Vladimir Putin ameitaka serikali yake "kuchukua hatua  dhidi ya muziki wa kufoka foka ama rap

 

Japo matamasha kadhaa ya muziki huo yamezuiwa katika maeneo mbalimbali ya nchi hiyo katika siku za hivi karibuni, jitihada za serikali kuupiga marufuku kabisa zimegonga mwamba.

 

Sababu marufuku ya serikali imeshindikana, Putin anataka mamlaka zifanye kazi ya ziada kuudhibiti.

 Putin amesema "Wizara ya Utamaduni itatafuta namna bora ya kusimamia matamasha ya vijana," 

 

Kauli ya Putin inakuja siku chache baada mwanamuziki wa maarufu wa rap nchini humo anayefahamika kama Husky kukamatwa baada ya matamasha yake kufutwa.

 

Awali mwezi huu wa Disemba mamlaka katika jiji la kusini la

Krasnodar zilizuia tamasha la Husky kwa kile walichokiita "msimamo mkali".

 

Mwanamuziki huyo ambaye jina lake halisi ni Dmitry Kuznetsov - alikonga nyoyo za mashabiki wake kwa kutumbuiza kutoka juu ya gari.

 Hata hivyo alikamatwa na kufungwa jela kwa siku 12 kwa kitendo hicho

 

Akizungumza katika mkutano wa Baraza la Utamaduni na Sanaa katika jiji la St Petersburg, rais Putin amesema "tatizo hili linapaswa kutatuliwa kwa umakini mkubwa".

 "Kile ambacho ninakubaliana nacho ni kuwa, kama ni ngumu kuuzuia (muziki wa rap), basi inabidi uongozwe kwa namna yake," amesema

 

Putin ameelezea hofu yake juu ya matumizi ya mihadarati kwa vijana.

 

"Rap na aina nyingine za kisasa za sanaa zimejikita katika nguzo tatu- ngono, mihadarati na maandamano," na 

"Ninaogopa zaidi mihadarati, maana hiyo ndio njia ya kuangamiza taifa. Putin amesema

 Serikali ya Urusi imekuwa na mahusiano ya kutatanisha na muziki kwa muda mrefu.

 

Bendi ya muziki ya Pussy Riot ambayo ni maarufu kwa kuukosoa utawala wa Putin imedai kuwa shirika la ujasusi la nchi hiyo lilimdunga sumu mwana bendi hiyo Pyotr Verzilov mwezi Septemba mwaka huu.

 

 

Chini ya Usovieti, aina za muziki za Magharibi kama pop na rock zilikuwa ni marufuku na baadhi ya wanamuziki wa Kirusi waliofanya aina hizo za muziki walikabiliana na mkono wa sheria.

 

Hata wale waliofanya muziki wa asili pia waliingia kwenye migogoro na serikali.

Mwanamuziki Dmitri Shostakovich alipigwa marufuku mara mbili chini ya utawala wa Joseph Stalin.

 joseph stalin

 

www.mzunguko.com

 

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon