Nchi ya Bangla Desh inashinda vita na kupata uhuru kutoka Pakistan mwaka 1971

December 16, 2018

Bendera ya Bangla Desh

[tarehe16 mwezi wa 12 mwaka 1971 tukio hili la Bangladeshi kupata uhuru kutoka pakistani linatokea]

Bangladesh ni nchi ya Asia ya Kusini imepakana na uhindi pande zote za barani isipokuwa mpaka mfupi wa km 193 na Myanmar upande wa kusini-mashariki na pwani ya ghuba ya bengali.

 Bangladesh ni sehemu ya mashariki ya Bengali ya kihistoria ambayo ilikuwa ndani ya Uhindi wa Kiingereza hadi 1947

 

Mwaka 1857 Wahindi walipinga utawala wa Kampuni ya Kiingereza kwa Uhindi wa Mashariki. Matokeo yake utawala ulishikwa na serikali yenyewe ya Uingereza kama koloni (1858)

 

.Mwisho wa karne ya 19 harakati za Wahindi kutafuta uhuru zilianza upya. Mwaka 1885 chama cha INC (Indian National Congress) kiliundwa na Wahindu na Waislamu pamoja waliodai uhuru

 

Mwaka 1906 viongozi Waislamu walitoka katika INC na kuunda "Shirikisho la Waislamu"

 

Mwaka 1917 Uingereza ilitamka ya kwamba ilitaka kuelekea polepole hali ya kujitawala kwa Wahindi. Viongozi wa wenyeji hawakuridhika na mkasi wa mabadiliko.

 

Chini ya uongozi wa Mahatma Ghandi mwendo wa kupigania uhuru bila mabavu ulipata nguvu.

 

Ghandi alipigania hasa umoja wa Wahindu na Waislamu lakini alipingwa na viongozi wenye itikadi kali wa pande zote mbili

 

 

Baada ya Vita Kuu ya Pili ya Dunia Waingereza walikubali kujiondoa katika Uhindi.

Swali kubwa lilikuwa kama nchi itabaki kama nchi moja au kama maeneo ya Waislamu yatajitenga

 

Tarehe 14/15 Agosti 1947 utawala wa Uingereza ulikwisha. Bara Hindi liligawanywa katika nchi mbili za Uhindi na Pakistan. 

Mgawanyo wa Uhindi ulikuja na vita vya  kumwaga  damu nyingi.

 Bengali yenyewe iligawanyika kwa sababu wakazi wengi wa mashariki walikuwa Waislamu, tofauti na Wabengali wengine waliokuwa Wahindu.

 Tarehe 30 Januari 1948 Ghandi mwenyewe aliuawa na Hindu mkali aliyemchukia kwa sababu alitaka usawa wa Waislamu na Wahindu.

 Wakati ule Bengali ya mashariki ilikuwa nchi moja pamoja na Pakistan ya leo, bila kujali umbali mkubwa kati ya pande hizo mbili zilizounganishwa na dini.

 Iliitwa "Pakistan ya Mashariki" mpaka mwaka 1971 ilipojitenga na Pakistan kwa msaada wa India katika Vita vya Uhuru vya Bangla Desh.

 

www.mzunguko.com

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon