Je wajua neno falsafa ni pendo la hekima

December 17, 2018

 Wanafalsafa Plato na Aristoteli; uchongaji wa karne ya 15 kwenye mnara wa kanisa huko Firenze, Italia.

 

KWANINI  TUNASEMA FALSAFA NI PENDO LA HEKIMA

 

 Neno lenyewe Falsafa linajieleza kwa ufasaha kuwa ni jaribio la kuelewa na kueleza ulimwengu kwa kutumia akili inayofuata hoja za mantiki.

 

Falsafa pia huchunguza mambo kama kuweko na kutokuweko ujuzi,uzuri, mema na mabaya, lugha, haki na mengine yoyote.

 

Tofauti na dini, imani au itikadi, njia ya falsafa ni mantiki inayoeleza hatua zake ikiwa tayari kuchungulia upya kila hatua iliyochukua.

Kwa hiyo falsafa ni njia ya kuuliza maswali na kutafuta majibu.

Katika lugha ya kila siku neno "falsafa" mara nyingi linachukuliwa kutaja jumla ya mafundisho au imani ya mtu au kundi la watu,

 

kwa mfano "falsafa ya chama fulani", "falsafa ya maisha yangu" na kadhalika. Lakini kwa jumla fikra hizo hazistahili kuitwa "falsafa". Ila tu kuna makundi ya wanafalsafa wanaopendelea mielekeo tofauti na kuhusu haya inawezekana kutumia neno "falsafa ya fulani" kwa kutaja matokeo ya kazi yao

Kuna mbinu nyingi za falsafa zilizoendelea kulingana na mazingira ya utamaduni ambako wanafalsafa waliishi.

 

Mara nyingi falsafa imeendelea karibu na dini, ndani ya dini au kwa mchanganyiko na dini mbalimbali.

 Lakini falsafa inachunguza pia matamko ya dini na kuuliza maswali juu ya maana ya matamko haya.

 

Wanafalsafa muhimu wa Asia walikuwa Konfutse na Lao Tze katika China na Buddha katika Uhindi.

 

Chanzo cha falsafa katika Ulaya kilitokea katika ustaarabu wa Ugiriki ya Kale.

 

Wanafalsafa wa huko waliweka misingi mingi kwa dunia ya baadaye pamoja na misingi ya sayansi ya sasa.

 

Kati ya majina mashuhuri ni Plato na Aristoteli

 

 

www.mzunguko.com

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon