Baada ya vuta ni kuvute ya wiki mbili muafaka wafikiwa COP24


Baada ya wiki mbili za majadiliano ya makundi zaidi ya 200 yaliyokusanyika Katowice, Poland kwa ajili ya mkutano wa Umoja wa Mataifa wa mabadiliko ya tabianchi , COP24,

yameidhinisha muongozo wa utekelezaji wa mkataba wa Paris wa mwaka 2015, wenye lengo la kupunguza ongezeko la joto duniani kuwa chini ya nyuzi joto 2 ikilinganishwa na viwango kabla ya wakati wa viwanda.

Taarifa kutoka Katowice, Poland, iliyotolewa, inasema kuwa mkataba umeridhiwa baada ya majadiliano ya usiku kucha

na hatimaye kukasikika shangwe na vigegele kumkaribisha rais wa mkutano wa COP24, Michal Kutyka, akifungua kikao cha mwisho ambacho kilihahirishwa mara kadhaa

Rais huyo katika hotuba yake amewashukuru wajumbe waliokuwa wanamsikiliza katika chumba cha mikutano kwa kile alichokiita, “ ustahamilivu” akiweka bayana kuwa usiku uliopita ulikuwa , “mrefu sana”.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, katika hotuba yake iliyosomwa kwa niaba yake na mkuu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa ya mabadiliko ya tabianchi, Patricia

Espinosa,

amesema kuwa , Katowice imeonyesha kuwa kwa mara nyingine tena mnepo wa mkataba wa Paris ambao ni ramani ya hatua dhidi ya mabadiliko ya tabianchi.

Bw. Guterres ambaye amegusia suala la athari za mabadiliko ya tabianchi kama moja ya mkakati wake kwa muhula huu kama Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa.

Alihudhuria mkutano wa Katowice mara tatu katika kipindi cha wiki tatu zilizopita ili kuunga mkono majadiliano hayo,

lakini kutokana na kuahirishwa kwa mara kadhaa alilazimika kuondoka kabla ya kikao cha mwisho kutokana na shughuli zingine zilizomsubiri mahala pengine

www.mzunguko.com


Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu