Mahakama yaamua kuwa obamacare inakiuka katiba

December 15, 2018

  Mahakama imesema kuwa bima ya obamacare inakiuka sheria

 

Jaji wa jimbo la Texas nchini Marekani ameamuru kuwa baadhi ya vipengele vya sheria katika bima ya afya maarufu kama Obamacare, vinakiuka katiba.​ 

 

Majimbo 26 yalihoji kuwa mwongozo wa sheria za bima hiyo umepitwa na wakati baada ya mswada wa ushuru kuidhinishwa kuwa sheria mwaka jana.

 

  Sheria hiyo mpya iliondoa faini dhidi ya watu ambao hawajajisajili kwa mpango huo wa afya

 

Rais wa Marekani Donald Trump amesema uamuzi huo ni habari njema kwa Wamarekani

 

Uamuzi huo unakuja siku moja kabla ya kumalizika kwa muda wa mwisho wa kujisajili kwa bima hiyo.

 Sheria inayoongoza bima hiyo hata hivyo itaendelea kutumika hadi uamuzi huo utakapo amuliwa na mahakama ya juu zaidi ya Marekani

 

Wakati wa kampeini yake ya Urais Trump aliahidi kufutilia mbali mpango huo wa Afya uliyobuniwa na mtangulizi Obama mwaka 2010, ili kuwapatia raia wa nchi hiyo bima ya afya ya gharama nafuu

 

Licha ya chama cha Republican kuwa na wabunge wengi katika mabunge yote mawili imeshindwa kufutilia mbali Obamacare

 

Hata hivyo mwaka 2017 bunge lilifanyia marekebisho bima hiyo ili kuwaruhusu wafanyibiashara wadogo na watu binafsi kuungana na kuanzisha miungano na kufadhili usimamizi wa bima mbadala kulingana na sheria ya majimbo yote ya Marekani

 Baadhi ya majimbo ya Marekani yanahoji kuwa kufutilia mbali mpango huo kutawaathiri mamilioni ya watu nchini humo.

  Kiongozi wa Demokratic katika bunge la seneti Chuck Schumer amesema: "Uamuzi huo mbaya ukidumishwa katika mahakama ya juu itakuwa ni pigo kwa mamilioni ya familia za Marekani."

 

www.mzunguko.com

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon