Uchaguzi DRC 2018: Kwa nini huenda Rais Joseph Kabila akawania urais tena 2023


Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Joseph Kabila amesema ataendelea kushiriki katika siasa nchini humo hata baada ya kuondoka madarakani baada ya uchaguzi utakaofanyika wiki mbili zijazo

Aidha, hajafutilia mbali uwezekano wake wa kuwania tena urais uchaguzi mkuu mwingine utakapoandaliwa mwaka 2023.

Bw Kabila alitarajiwa kuondoka madarakani miaka miwili iliyopita baada ya kuongoza kwa mihula miwili kwa mujibu wa katiba.

Hata hivyo, uchaguzi mkuu nchini humo uliahirishwa mara kadha, serikali ikisema maandalizi yake hayakuwa yamekamilika vyema.

Upinzani ulitazama hilo kama njama ya Bw Kabila kutaka kuendelea kuongoza

Mwezi Agosti, Bw Kabila alimtangaza mshirika wake wa karibu Emmanuel Ramazani Shadary ambaye ni waziri wa zamani wa mambo ya ndani kuwa mgombea wa muungano wa kisiasa unaotawala kwa sasa.

Bw Shadary amewekewa vikwazo na Umoja wa Ulaya kutokana na tuhuma za ukiukaji wa haki za kibinadamu.

Katibu wa chama cha upinzani cha Movement for the Liberation of Congo (MLC), Eve Bazaiba, amesema kwamba Bw Shadary atadhibitiwa na Bw Kabila na kwamba kimsingi itakuwa ndiye anayeongoza nchi.

"Anataka tu kusalia madarakani. Hata kama alimchangua Shadary, Shadary ni mtu tu wa kuonekana, ndiye atakayemuongoza Shadary kwa kila jambo. Kiuhalisia, atakuwa bado ndiye rais."

Bi Bazaida amesema serikali imekuwa ikiwazuia wanasiasa wa chama cha MLC kufanya kampeni

Kwa muda mrefu, ilikuwa bado haijabainika iwapo Rais Kabila, angewania tena hadi alipoamua kumtangaza Shadary kuwa mgombea wa muungano wake wa kisiasa

www.mzunguko.com


Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu