Tetesi za Soka Ulaya Jumapili 09.12.2018: Kane, Hazard, Suarez, Fabregas, Welbeck, Carroll

December 9, 2018

Barcelona watamfanya mshambuliaji wa Tottenham na England anayewekewa thamani ya pauni milioni 200 mwenye miaka 25 Harry Kane kuwa lengo lao kuu msimu ujao

 

Paris St-German wanataka kumsani mchezaji mweye miaka 25 wa Chelsea raia wa Ubelgiji Eden Hazard msimu ujao lakini watakabiliwa na ushindani kutoka Real Madrid na Juventus. 

 

Manchester United watahitajika kulipa pauni milioni 90 kwa mchezaji wa Napoli beki mwenye miaka 27 raia wa Senegal Kalidou Koulibaly ambaye Jose Mourinho anamlenga sana mwezi Januari.

Chelsea wanamfuatilia kiungo wa kati wa Barcelona na Uhispania Denis Suarez. Ikiwa mchezaji huyo wa miaka 24 ataelekea Stamford Bridge, Blues watamruhusu mwenzake Cesc Fabregas, 31, kujiunga na AC Milan. 

 

Straika wa England Danny Welbeck, 28, ataachiliwa na Arsenal wakati mkataba wake utakamilika mwisho wa msimu na kupewa fursa ya kujiunga na Galatasaray.

 

Tottenham pia wamehusishwa na kiungo wa kati wa Feyenoord na Netherlands Tonny Vilhena, 23, ambaye analengwa na Roma. 

 

Straika wa West Ham na England Andy Carroll, 29, anataka kukaa zaidi ya msimu huu wakati mkataba wake utakamilika. 

 

Manchester United wamefanya mazungumzo na Amiens wanapojaribu kukubaliana fidia kwa mshambuliaji mfaransa wa kikosi cha chini ya miaka 16 Mfaransa Noam Emeran.

 

Mchezaji huyo pia anamezewe mate na Paris St Germain na Juventus

 www.mzunguko.com

 

 

 

 

 

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon