Hatua za kupambana na ajali za barabarani hazitoshi-WHO


Shirika la afya ulimwenguni WHO limesema hakuna hatua kubwa zilizopigwa katika kukabiliana na changamoto ya usalama barabarani kote duniani.

Kwa mujibu wa ripoti mpya ya WHO iliyozinduliwa leo mjini Geneva Uswis, vifo vitokanavyo na ajali za barabarani vinaendelea kuongezeka na kufikia vifo milioni 1.35 kwa mwaka

Ripoti hiyo ambayo ni “Mtazamo wa kimataifa wa WHO kuhusu usalama barabarani 2018” unaeleza kwamba majeraha yatokanayo na ajali za barabarani sasa ndio chanzo kinachoongoza kwa vifo vya watoto na vijana wa kati ya umri wa miaka 5 hadi 29

Akisisitiza haja ya kukabiliana na tatizo la ajali hizo mkurugenzi mkuu wa WHO Dkt. Tedros Adhanom Ghebreyesus amesema “Vifo hivi ni gharama isiyokubalika katika safari,

hakuna kisingizio chochote kwa kutochukua hatua, hili ni tatizo ambalo lina suluhu. Ripoti hii ni wito kwa serikali na wadau wote kuchukua hatua zaidi kutekeleza mikakati hiyo.

Ripoti hiyo pia imesema licha ya idadi ya vifo kuongeza , kiwango cha vifo kulingana na idadi ya watu duniani kinaonekana kutokuwa kikubwa sana kwa miaka ya karibuni, hii ikiaashiria kwamba juhudi zilizopo za usalama barabarani katika nchi za kipato cha wastani na kipato cha juu zimesaidia.

Ripoti imeongeza kuwa katika sehemu ambako hatua zimepigwa kwa kiasi kikubwa ni kwa sababu ya será nzuri katika masuala ya hatari kama vile

mwendo wa kasi kupita kiasi, kulewa na kuendesha,magari, kutofunga mikanda, kutovaa helmeti kwa waendesha pikipiki, kutowalinda watoto, miundombinu salama kama kuwa na sehemu maalumu ya waendesha baiskeli na watembea kwa miguu, kuboresha viwango vya ubora wa magari ikiwemo breki na pia kuboresha huduma za baada ya ajali.

Kwani ripoti inasema hatua hizi zimesaidia kupunguza vifo vitokanavyo na ajali za barabarani katika nchi 48 za kipato cha kati na za kipato cha juu. Hata hivyo imeonya kwamba hakuna hata nchi moja ya kipato cha chini iliyoonyesha kupunguza idadi ya vifo kwa ujumla na kwa asilimia kubwa ni kwa sababu hatua hizi zinakosekana

Kwa mantiki hiyo ripoti inasema “hatari ya vifo vya ajali za barabarani katika nchi za kipato cha chini ni mara tatu zaidi ya ilivyo katika nchi za kipato cha juu, na viwango hivyo ni vikubwa zaidi barani Afrika ambapo ni uwiano wa watu 26.6 kwa kila watu 100,000 na kiwango kidogo zaidi ni barani Ulaya ambako ni uwiano wa watu 9.3 kwa kila watu 100,000.”

www.mzunguko.com


Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu