Je wajua kanisa kubwa mjini Istanbul lililobadilishwa kuwa msikiti tangu mwaka 1453

December 7, 2018

Hagia Sophia ni jina la Kigiriki la kanisa kubwa mjini Istanbul Konstantinopoli lililobadilishwa kuwa msikiti tangu 1453 na halafu kuwa makumbusho mwaka 1934

Hagia Sophia kwa ndani

 

Ujenzi wa kanisa ulianzishwa mwaka 532 na Kaisari Justiniani I mtawala wa Roma ya Mashariki au Ufalme wa Byzanti

Alitaka kuwa na kanisa kubwa kuliko yote duniani akafaulu kwa sababu Hagia Sofia ulikuwa ukumbi mkubwa duniani hadi mwaka 1520

Sanamu ya Yesu katika ukuta wa Hagia Sophia

 

Jengo lilikamilishwa baada ya miaka mitano na Justiniani alipoingia mara ya kwanza aliita "Suleimani nimekushinda", akimfikiria mfalme Suleimani wa Israeli ya Kale aliyejenga hekalu la Yerusalemu.

 

Mwaka 1453 Waturuki Waislamu waliteka mji wa Konstantinopoli na kuifanya mji mkuu wa Dola la Osmani

Hagia Sophia mjini Istanbul

 

Hapo Hagia Sofia ikabadilishwa kuwa msikiti na Waturuki wakatamka jina la kigiriki kama "Ayasofya".

Jengo la kanisa likaongezewa minara minne ya mtindo wa Kiislamu.

 Baada ya anguko la Waosmani katika vita kuu ya kwanza ya dunia kiongozi wa taifa Kemal Atatürk akaamuru jengo liwe makumbusho

 

www.mzunguko.com

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon