Mchungaji wa kiprotestanti, kutoka ujerumani Anton Praetorius aliyepiga vita desturi mbaya ya kushtaki watu kwa kuwa wachawi alifariki mwaka 1613

December 6, 2018

 [Siku kama ya leo tarehe 6 mwezi wa 12  mwaka wa 1613, Anton  Praetorius  mchungaji  kutoka ujerumani alifariki huku akiacha kumbukumbuku katika taifa la ujerumani  kuwa kiongozi wa dini  aliyekuwa akipiga vita mateso  kwa  wale walioshtakiwa ili yaondolewe]

1586 mke wake Mariamu alijifungua mtoto wa kiume, jina lake aliitwa Yohana

1595 Praetorius alitunga shairi juu ya Pipa kubwa katika Boma la Heidelberg

 

1596 alipata kuwa mchungaji binafsi wa mtawala fulani huko Birstein karibu na Frankfurt/Main​ 

 

1597 Praetorius alileta udaku mkali barazani ili kupinga mateso ya mama fulani aliposhtakiwa kuwa mchawi. Hakimu hakuendelea kumshtaki yule mama akafunga shauri. Mama huyo aliachishwa huru.

Lakini Praetorius aliachishwa kazi yake kama mchungaji wa pale

1598 Praetorius alipata kuwa mchungaji wa usharika wa Laudenbach/Bergstrasse.

 

Aliandika kitabu Ripoti juu ya Uchawi na Wachawi. Katika kitabu hicho alileta udaku ili iondolewe ile desturi mbaya ya kuwaonea watu kuwa wachawi, tena yaondolewe mateso.

 

Alikiandika kitabu hicho akitumia jina la fumbo Yohana Scultetus lililokuwa jina la mwanawe

 

1602 na 1613 alikichapa kitabu chake tena, lakini mara hii alitumia jina lake la kweli. Toleo la pili 1602, na la tatu 1613.

 1629 alipokuwa amekwisha kufa toleo la nne  juu ya Uchawi na Wachawi lilichapwa.


 www.mzunguko.com

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon