'Marekani ikitengeneza makombora sisi pia tutatengeneza' aonya rais Putin

December 6, 2018

Rais Putin  amesema Urusi itatengeneza makombora iwapo Marekani itajiondoa katika mkataba unaodhibiti silaha hizo.

Urusi itaunda makombora yaliyopigwa marufuku chini ya mkataba wa vita baridi ikiwa Marekani itajiondoa katika mkataba unaodhibiti silaha hizo, ameonya rais Vladimir Putin

 

Tamko lake linakuja baada ya shirika la kujihami kwa mataifa ya magharibi Nato, kuilaumu Urusi kwa kukiuka mkataba wa makubaliano kudhibiti uundaji wa makombora ya masafa ya kadri (INF).

 

Makubaliano hayo yaliyotiwa saini mwaka 1987 kati ya Marekani na USSR,yalipiga marufuku mataifa hayo yote mawili dhidi ya kuunda makombora ya masafa mafupi na yale kadri 

Rais wa Putin amesema tuhuma za Nato dhidi ya taifa lake ni kisingizio cha Marekani kujiondoa katika mkataba huo.

 

Katika tamko hilo lililoangaziwa kwenye televisheni, kiongozi huyo alisema mataifa mengi yanaunda silaha zilizopigwa marufuku katika mkataba wa INF

 

"Sasa inaonekana kuwa washirika wetu Marekani wanahisi kwamba mambo yamebadilika sana kiasi cha kuwa wanaona ni lazima wao pia wawe na silaha ," alisema.

 "Jibu letu ni nini? Bila shaka - sisi pia tutafuata mkondo huo.

 Rais wa Marekani Donald Trump siku za hivi karibuni aligusia kuwa taifa hilo huenda likajiondoa katika mkataba huo kutokana na mienendo ya Urusi

 

www.mzunguko.com

 

 

 

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon