Je wajua kiwanja cha kale mjini Roma kilichokuwa kinaonyesha maonyesho ya watu au wanyama wakiuawa kikatili

December 6, 2018

Koloseo [kiitalia;colosseo] ni kiwanja cha michezo cha kale mjini Roma nchini italia kilichopo katika hali ya maghofu kutokana na umri wake  wa miaka 2000, ni kati ya majengo mashuhuri mjini Roma na Duniani kwa ujumla

Koloseo mwaka 2007 wakati wa usiku

 

Wakati wa Dola la Roma koloseo  ilikuwa   jengo kubwa kabisa lililojengwa na Waroma wa kale.

koloseo ilijengwa kuanzia mwaka 70 hadi 80 BK.

 

Kaisari Vespasiano alianzisha ujenzi kwa kutumia  mapato ya uwindo  wa vita  vya Waroma dhidi ya uyahudi na hasa  hazina ya hekalu ya Yerusalemu

Kiwanja kilikuwa  na nafasi kwa  watu 45,000 hadi 50,000.

 

Watazamaji waliangalia maonyesho ambayo  watu  au wanayama waliuawa, michezo hii iligharamiwa na serikali kwa ajili ya wakazi wa mji kama burudani.

falsafa ya kisiasa ya Roma ilisema ya kwamba watu watulia wakipewa ‘’panem  et  circenses’’ yaani  ''chakula na michezo’’

 Baada ya ushindi wa ukristo mashindano ya kuua watu yalipingwa na kanisa, na shindano la mwisho lilitokea mwaka 434/435.

mapigano dhidi ya wanyama yaliendelea hadi mwaka  523, lakini baada ya  mwisho wa Dola  la Roma  idadi ya wakazi wa Roma  ilipungua na  koloseo haikutumiwa  tena kwa michezo

 

MICHEZO KATIKA KIWANJA CHA KALOSEO

 

michezo katika  kaloseo ilikuwa ya aina  mbili

 

1.mashindano ya wapiganaji walioshindana kwa silaha za kweli hadi kifo.

 Sehemu ya  ndani ya Koloseo

 Wapiganaji waliitwa na Waroma kwa jina la "gladiator" yaani "mwenye upanga". Wengi wao walikuwa watumwa lakini wengine walikuwa watu huru.

 

Walijifunza mapigano kwa silaha kwa ajili ya maonyesho na kuitumia kwenye kiwanja mbele ya watazamaji. Walioshinda walipata tuzo na zawadi nyingi. Wegine walikufa na kusahauliwa.

 

2.mashindano kati ya watu na wanyamapori.

 

Waroma wa Kale walikamata wanyamapori kutoka Ulaya na Afrika ya Kaskazini kwa ajili ya maonyesho hayo.

 

Wanyama waliuawa na magladiator kwenye kiwanja mbele ya watazamaji, lakini ilitokea pia ya kwamba wawindaji waliuawa na wanyama

 wakristo jinsi walivyowekwa mbele ya simba

 

Tangu karne ya 3 Wakristo waliuawa kiwanjani kama sehemu ya maonyesho.

 

Ukristo ulikuwa dini marufuku katika Roma ya Kale hadi mwaka 313.

 

Wakati mwingine Wakristo walikamatwa kwa wingi na kupewa adhabu ya kifo.

 

Walionekana walifaa kwa maonyesho ambako walisimamishwa mbele ya wanyamapori kama simba, chui au dubu.

 

www.mzunguko.com

 

 

 

 

 

 

 

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon