Tetesi za Soka Ulaya Jumatano 05.12.2018: Pogba, Fabinho, Ibrahimovic

Juventus wanatafakari kuweka dau la kumnunua Paul Pogba,25, kiungo wa kati wa Manchester United na timu ya Taifa ya Ufaransa

Pogba

Meneja wa Manchester United Jose Mourinho amekataa kutoa taarifa ya kikosi chake kitakachominyana na mahasimu wao wa jadi Arsenal usiku wa leo Jumatano

Kiungo wa kati wa Ureno Andre Gomes anayechezea klabu ya Everton kwa mkopo hajaonesha nia ya kutaka kurudi Barcelona

Everton sasa inapania kutumia uamuzi wa kiungo huyo wa miaka 25 kuimarisha dau lake kwa lengo la kumpatia mkataba wa kudumu

kiungo wa kati wa Liverpool na Brazil Fabinho, 25, amesema haoni sababu ya kujiunga na Paris St-Germain mwezi Januari mwakani licha tetesi kuwa huenda akahamia klabu hiyo ya Ufaransa

Mshambuliaji wa LA Galaxy na Sweden Zlatan Ibrahimovic, 37, huenda akarejea AC Milan hivi karibuni bada ya mazungumzo kuhusiana na mpango huo kushika kasi

Meneja wa Monaco Thierry Henry anataka kumsajili mshambuliaji wa Italia Stefano Okaka, 29 ambaye hana raha tena ya kusalia Vicarage Road

Manchester City huenda ikamnunua winga wa Leeds United Jack Clarke 18, mwezi January.

Fulham,Crystal Palace na West Ham wanafuatilia mchezo wa mshambuliaji wa Nantes na Argentina Emiliano Sala, 28

www.mzunguko.com


Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu