Nukuu za laozi, mmoja wa wanafalsafa mashuhuri nchini china aliyeishi karne ya 6 kk


Laozi alishi katika karne ya 6 KK lakini Laozi si jina bali cheo kama "mwalimu".

Anajulikana hasa kutokana na kitabu cha Tao te jing kinachotajwa kama kazi yake.

Anatazamwa kama mwanzilishi na mwalimu mkuu wa Utao ambao ni fundisho linalopatikana kama falsafa na pia kama dini. Katika matawi ya kidini ya Utao anatazamwa kama mungu mmojawapo

Kuna nukuu nyingi zinazoaminiwa kuwa za Laozi. Hata hivyo wataalamu wengi wanaoamini ya kwamba masimulizi juu yake yametungwa karne nyingi, pamoja na kuwa na mashaka kama kweli mtu huyu aliishi, hali halisi wanasita kukubali nukuu.

Baadhi ya nukuu zinazopatikana katika jina lake ni kama zifuatazo

1.Kiongozi bora ni yule ambaye watu hawana habari nyingi juu yake; akimaliza kazi yake wengine watasema "ni sisi wenyewe tuliofanya yote"

2.ongoza milki kubwa kwa mkono wa upole jinsi unavyopika samaki wadogo

3.Tatizo kubwa kabisa duniani lingepata suluhisho kirahisi wakati lilikuwa bado dogo na changa.

www.mzunguko.com


Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu