kumbukumbu ya kifo cha rais wa kwanza wa Afrika kusini aliyechaguliwa kidemokrasia katika nchi yake, Nelson Mandela alifariki mwaka 2013

December 5, 2018

 [siku kama ya leo tarehe 5 mwezi wa 12 katika mwaka wa 2013  tunakumbuka kifo cha Nelson mandela  aliyekuwa Rais wa kwanza wa afrika kusini aliyechaguliwa kidemokrasia na wananchi wake na aliyepambana dhidi ya ubaguzi wa rangi nchini afrika m kusini]

Alikuwa mwanasheria na mwanachama, baadaye kiongozi wa chama cha ANC kilichopigania haki za binadamu wote nchini Afrika Kusini

HARAKATI ZA UBAGUZI WA RANGI

 

Mandela alihukumiwa kifungo cha maisha kwa miaka 27 kutokana na harakati zake za kuupinga ubaguzi wa rangi. Alifungwa katika kisiwa cha Robben.

 

Baada ya kuachiliwa huru mwaka 1990 alianzisha sera ya maridhiano au sera ya amani baina yake na watu weupe nchini Afrika Kusini, jambo ambalo watu wengi hawakulitegemea.

 

Mwaka wa 1993, pamoja na Frederik Willem de Klerk alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Amani ambayo ni tuzo ya nadra kutolewa duniani.

 

Baada ya kutengana na mke wake, Winnie Madikizela, alimuoa Graca Machel aliyewahi kuwa mke wa rais wa Msumbiji, Samora Machel.

 

www.mzunguko.com

 

 

 

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon