Msanii wa hip hop na mfanyabiashara kutoka nchini Marekani anayefamika zaidi kwa jina lake kama Jaz-

[ siku kama ya leo, tarehe 4 mwezi wa 12 mwaka wa 1969 msanii Jaz-z alizaliwa]

Shawn Corey Carter amezaliwa tar. 4 Desemba 1969 ni msanii wa hip hop na mfanyabiashara kutoka nchini Marekani.

Anafahamika zaidi kwa jina lake la kisanii kama Jay-Z. Huyu ni Ofisa Mkuu wa zamani wa Def Jam Recordings na Roc-A-Fella Records

Pia ni mmoja kati ya wanaomiliki klabu ya The 40/40 Club na New Jersey Nets.

Huyu ni mmoja kati ya wasanii na mjasiriamali wa hip hop wa Marekani wenye mafanikio makubwa kabisa, kwa kuuza nakala zaidi ya milioni 26 nchini Marekani na kupokea Tuzo za Grammy kadhaa kwa kazi zake za kimuziki

Pamoja na kuwa na mafanikio yake makubwa ya kimuziki, Jay-Z anafahamika zaidi kwa kujihusisha na masuala ya ugomvi na baadhi ya wasanii wengine wa soko zima la rap,

moiongoni mwa ugomvi mkubwa uliokuwa unajulikana na watu wengi duniani ni ule wa yeye na rapa mwenziwe wa mjini New York Bw. Nas, ambao ulikuja kusuluishwa mnamo mwaka wa 2005.


Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu