Mark Hughes: Southampton wamfuta meneja wao baada ya miezi minane kufuatia sare na Manchester United

Meneja wa Mark Hughes amefutwa kazi baada ya kuhudumu kama meneja wa Southampton kwa miezi minane pekee

Watakatifu hao wa St Mary's, waliotoka sare na Manchester United katika Ligi ya Premia Jumamosi, kwa sasa wanashikilia nafasi ya 18 kwenye jedwali.

Southampton wamethibitisha kufutwa kwake kupitia taarifa, na kuongeza kwamba : "Mchakato wa kumtafuta meneja mpya wa kuipeleka mbele klabu hiyo tayari umeanza."

Mkufunzi msaidizi wa kikosi cha kwanza Kelvin Davis ataongoza timu hiyo kwa mechi yao dhidi ya Tottenham siku ya Jumatano.

Hughes, ambaye aliwahi kuchezea klabu hiyo ya pwani ya kusini mwa England, alijiunga na Southampton mwezi Machi,

Southampton walikuwa alama moja juu ya eneo la kushushwa daraja wakati huo na mkufunzi huyo wa miaka 55 aliwaongoza kujinusuru kwa kuwawezesha kushinda mechi mbili kati ya mechi zao nne za mwisho.

Kabla ya kutoka sare na Manchester United, Southampton walicharazwa 3-2 na Fulham ambao pia wanakabiliwa na hatari ya kushushwa daraja. Aidha, waliondolewa

Kombe la Ligi kwa mikwaju ya penalti na Leicester City.

Pamoja na Hughes, meneja msaidizi wa kikosi cha kwanza Mark Bowen na mkufunzi Eddie Niedzwiecki pia wameondoka klabu hiyo


Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu