Je wajua neno la Kiswahili linalojumlisha idadi kadhaa ya Hisia kuanzia mahaba,pendo hata upendo wa


Mapenzi ni neno la Kiswahili linalojumlisha idadi kadhaa ya hisia, kuanzia mahaba, pendo hata upendo wa Kimungu.

Neno "kupenda" linaweza kurejelea aina za hisia, hali na mitazamo tofautitofauti, kuanzia ridhaa ya jumla ya kitu("Napenda chakula hiki"), hadi mvuto mkali kati ya binadamu ("Nampenda mume wangu")

mapenzi kwa kawaida yanarejelea hisia za ndani, zisizoelezeka, za kudumu kwa mtu mwingine.

Hata hivyo, maelezo haya yanashirikisha hisia tofauti, kutoka hamu na urafiki wa kimahaba hadi ukaribu wa kihisia wa kifamilia , usioelekea kabisa katika ngono,

Msingi wa kisaikolojia

Saikolojia inaonyesha mapenzi kama jambo tambuzi na la kijamii.

Mwanasaikolojia Robert Sternberg alibuni nadharia ya miraba mitatu ya mapenzi akasema mapenzi yana vipengele vitatu tofauti:

urafiki, kujitoa, na uchu.

Urafiki ni aina ambayo watu wawili huambiana siri na mambo kadhaa kuhusu maisha yao binafsi.

Kuwajibika, kwa upande mwingine, ni matumaini kuwa uhusiano huo ni wa kudumu.

Aina ya mwisho na inayopatikana sana ni mvuto wa kingono au uchu.

Mapenzi ya uchu ni kama yanavyoonyeshwa katika kupumbazwa kimapenzi pamoja na mapenzi ya kimahaba.

Aina zote za mapenzi hutazamwa kama mchanganyiko tofauti wa vipengele hivi vitatu.

www.mzunguko.com


Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu