Waziri mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu afunguliwe mashtaka ya ufisadi

Polisi nchini Israel wamependekeza kufunguliwa mashtaka kwa waziri mkuu Benjamin Netanyahu na mke wake Sara kwa madai ya ulaghai na ufisadi.

Wanashukiwa kuipendelea kampuni ya mawasiliano ya Bezeq telecom ili nayo iweze kuwapendelea kwa kuandika taarifa nzuri kuwahusu

Bw Netanuyahu alikana madai hayo yanayojulikana kama Case 4000

Mwanasheria mkuu nchini Israel sasa ataamua ikiwa ataleta mashtaka kuhusu madai hayo.

Kwenye taarifa ya leo Jumapili Bw Netanyau alisema: "Mapendezo haya yalifuja hata kabla ya uchunguzi kuanza.

"Nina uhakika kuwa katika kesi hii, mamlaka zinazoangalia suala hili zitafikia uamuzi ule ule kuwa hakuna chochote''

Mwezi Februari polisi walipendekeza kufunguliwa mashtaka Bw Netanyahu katika kesi zingine mbili za ufisadi.

Ametupilia mbali madai yote kuwa yasiyo na msingi.

Vyombo vya habari nchini Israel vinasema kuwa wachunguzi wamemhoji Netanyahu mara kadhaa.

Netanyahu, 69, anaongoza muungano tete lakini anaamini kuwa madai hayo hayawezi kuchochea uchaguzi wa mapema.

Uchaguzi wa bunge unapangwa kufanyika Novemba 19. Bw Netanyahu anahudumu awamu ya pili kama waziri mkuu.

www,mzunguko.com


Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu