Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Aliyekuwa kiongozi wa kijeshi na wa kisiasa nchini Ufaransa Napeleone Bonaparte mnamo mwaka wa 1804 tarehe 2 mwezi wa 12 anajiwekea taji la kuwa kaisari wa Ufaransa

December 2, 2018

Napoleon Bonaparte ofisini kwake. Picha ilichorwa na Jacques-Louis David, 1812

 

Napoléon Bonaparte (Napoleone di Buonaparte, alizaliwa tarehe 15 Agosti 1769 –  na kufariki tarehe 5 Mei 1821) alikuwa kiongozi wa kijeshi na wa kisiasa nchini Ufaransa baada ya mapinduzi ya Kifaransa.

Alizaliwa kwenye kisiwa cha Korsika akasomeshwa katika shule ya jeshi na kuwa mwanajeshi.

Wakati wa mapinduzi mwaka 1793 alijipatia sifa dhidi ya watetezi wa ufalme kwenye mji wa Toulon waliosaidiwa na Uingereza akapandishwa cheo na kuwa jenerali akiwa na umri wa miaka 24. 

 Mwaka 1796 alipewa amri ya jeshi la Ufaransa katika Italia akafaulu dhidi ya jeshi la Austria iliyopaswa kuwachia Wafaransa utawala wa Italia

VITA YA MISRI

Mwaka 1798 aliongoza uvamizi wa Ufaransa katika Misri kwa shabaha ya kukata mawasiliano kati ya Uingereza na koloni lake la Uhindi.

Jeshi la Ufaransa katika mapigano karibu na Piramidi

 

Alifaulu kushinda Wamisri lakini manowari zake ziliharibiwa na Waingereza katika mapigano ya Abukir.

 

mwaka 1799 Napoleon alipaswa kuacha jeshi lake nyuma na kujiokoa pekee yake kwa kurudi Ufaransa. Uvamizi wa Wafaransa ilikuwa muhimu kisayansi kwa sababu aliongozana na wataalamu waliochungulia majengo ya Misri ya kale na nchi kwa jumla.

MAPINDUZI YA KIJESHI YA MWAKA 1799

 

Katika Ufaransa Napoleon alifanya mipango pamoja na wanasiasa wengine wa kuchukua utawala. Tarehe 9 Novemba 1799 (ilikitwa 18 Brumaire katika kalenda ya mapinduzi ya Kifaransa) Napoleon aliongoza wanejeshi wakiingia mjini Paris na kufukuza bunge. Katiba mpya ilimfanya mtawala wa pekee mwenye cheo cha "Konsuli ya kwanzaa". Kwa umri wa miaka 30 alikuwa mtawala wa Ufaransa.

1802 Napoléon alirudisha utumwa katika koloni za Ufaransa kwa sabau za kiuchumi akasababisha mapinduzi ya Haiti yaliyoleta uhuru wa nchi ile.

Wafalme wa Ulaya waliendelea kuangalia jamhuri ya Ufaransa kwa wasiwasi kwa sababu ilikuwa nchi ya Ulaya kwanza iliyopindua utawala wa kifalme. Napoleon aliiuzia Marekani koloni za kifaransa katika Amerika ya Kaskazini (Lousiana na mji wa New Orleans) alipoona ya kwamba angeshindwa

kuzitetea kama vita ingerudi.


KAISARI WAUFARANSA

 

Mwaka 1803 Uingereza ilitangaza upya hali ya vita. Hii ilikuwa mwanzo wa vita za mfulolizo hadi mwisho wa utawala wake. Katika Ufaransa aliendesha kempeni ya kuimarisha uatwala wake.

Baada ya fitina nyingine na wafuasi wa familia ya mfalme aliyepinduliwa Napoleon aliamua kujiwekea taji. Lakini hakutumia cheo cha mfalme akajiwekea taji la "Kaisari ya Wafaransa" tar. 2 Desemba 1804. Mwaka uliofuata alipewa pia taji la mfalme wa Italia.

Napoleon ajiwekea taji la kuwa kaisari wa Ufaransa

 

www.mzunguko.com

 

 

 

 

 

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload