Mkutano 24 wa mkataba wa kimataifa wa mabadiliko ya tabia nchi COP 24:

December 1, 2018

Wakati kiwango cha joto kikiendelea kupanda duniani , hatua dhidi ya mabadiliko ya tabianchi zinazorota na fursa ya kulishinda jinamizi hili inaendelea kuwa finyu.

 

Jumapili wiki hii Umoja wa Mataifa utaanza majadiliano muhimu ya jinsi gani ya kushughulikia tatizo hilo kwa pamoja na kwa haraka,

 katika wiki mbili za mkutano wa 24 wa mkataba wa kimataifa wa mabadiliko ya tabianchi, COP 24 utakaofanyika mjini Katowice nchini Poland.

 

 Mjini katowice nchini poland

 

Maelfu ya viongozi wa dunia, wataalam, wanaharakati, wabunifu, sekta binafsi na wawakilishi kutoka asasi za kiraia na jumuiya za wenyeji watakusanyika ili kushughulikia mpango wa hatua za pamoja kwa minajili ya kutimiza ahadi muhimu iliyowekwa na nchi zote mjini Paris, Ufaransa miaka mitatu iliyopita.

 Mjini Paris Ufaransa

 

UNFCCC, UNEP, WMO, IPCC, COP 24, Mkataba wa Kyoto, Mkataba wa Paris.

 

Vifupisho hivi na majina haya ya maeneo yanawakilisha nyenzo za kimataifa na mikakati ambayo chini ya uongozi wa Umoja wa Mataifa ilianzishwa ili kusaidia kusongesha mbele hatua za kimataifa dhidi ya mabadiliko ya tabianchi.

 

Vyote vina jukumu muhimu katika kutuongoza sote kufikia malengo ya kuwa na mazingira endelevu yaliyo ya kuvutia na kupendeza katika uso wa Dunia.

Mwaka 1992, Umoja wa Mataifa uliandaa mkutano mkubwa mjini Rio de Janeiro ulioitwa Earth Summit, ambako mkakati wa mkataba wa mabadiliko ya tabianchi (UNFCCC) ulipitishwa.

 Mjini Rio de Janeiro nchini Brazil

 

 

Katika mkataba huo Mataifa yaliafikiana "kudhibiti kiwango cha gesi ya viwandani hewani” ili kuzuia kuingilia katika shughuli za binadamu kwenye mfumo wa hali ya hewa.  na mkataba huo umeridhiwa na Mataifa 197.

 Kila mwaka tangu mkataba huo uanze kutekelezwa mwaka 1994 “mkutano wa nchi wadau yaani COP unafanyika kujadili jinsi gani ya kusonga mbele na tangu hapo kumekuwa na mikutano 23 ya COP na mwaka huu kutakuwa na mkutano wa 24 au COP 24”

 www.mzunguko.com

 

 

 

 

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon