Je wajua chungwa ni kati ya matunda yanayovunwa sana Duniani

December 1, 2018

Chungwa ni tunda la mchungwa. Ni kati ya matunda yanayovunwa sana duniani. Jina la kisayansi ni Citrus aurantium L. var. sinensis L. au Citrus sinensis (L.) Osbeck

 Machungwa na maua yake 

 

Tunda lenyewe ni kijani na rangi inabadilika kuelekea njano ikiiva. Pamoja na limau, danzi, balungi na ndimu ni mojawapo kati ya matunda chungwa.

Siku hizi ni tunda linalovunwa zaidi kati ya matunda chungwa

Asili yake ni katika bara la  Asia ya Kusini-Mashariki ambako lilioteshwa na wakulima.

Kuna aina mbili  ya matunda chungwa yanayotofautiana kwa ladha  [chungu na  tamu]

Aina yenye ladha chungu iliwahi kusambaa duniani hivyo jina la Kiswahili limetunza ladha hii hata kama matunda mengi yanayopandwa siku hizi ni aina ya    chungwa tamu.

Chungwa tamu lilisambaa kote duniani baada ya Wareno kuchukua machipuko yake na kuyapanda kwanza Ureno baadaye hata Amerika na Afrika kuanzia karne ya 15.

 www.mzunguko.com

 

 

 

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon