Ndege ya kansela wa Ujerumani Angela Merkel ilitua ghafla kufuatia hitilafu ya kiufundi

November 30, 2018

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel atakosa ufunguzi wa mkutano wa G20  baada ya ndege yake kulazimika kutua muda mfupi baada ya kuondoka Berlin

 

Maafisa wa Bi Merkel na wajumbe wengine waliokuwa wamesafiiri kwenye  ndege hiyo  walitua salama mjini Cologne kutokana na matatizo ya kimitambo

 

Habari zaidi zinasema Merkel atasafiri mjini Buenos Aires leo( Ijumaa).

 

Hakuna taarifa zozote zilizotolewa kuhusiana na tatizo la kiufundi iliyokumba ndege hiyo.

 

Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, rubani aliwatangazia abiria kuwa ameamua kugeuza mkondo wa safari na kurudi alikotoka kufuatia kile alichosema kuwa "hitilafu ya mifumo kadhaa ya kielektroniki.

Ndege hiyo aina ya Konrad Adenauer ililakiwa uwanjani na magari ya kutoa misaada.

Ripoti zinasema Bi Merkel na ujumbe wa Ujerumani baadae walisafiri kwa basi hadi hoteli moja mjini Bonn.

 

Vyombo vya habari vya Ujerumani vimeongeza kuwa Kansela Merkel na waziri wake wa fedha, Olaf Scholz, wanatarajiwa kusafiri nchini Argentina baadae leo (Ijumaa

 

www.mzunguko.com

 

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon