Je wajua fani ya elimu jamii inayolenga kujua nafsi ya binadamu ili kurahisisha ukomavu wake na uhusiano wake na wenzake.

November 30, 2018

Elimunafsia  ni fani ya elimu jamii inayolenga kujua nafsi ya binadamu ili kurahisisha ukomavu wake na uhusiano wake na wenzake

Hakuna mtu wa jana, leo au kesho aliye sawasawa na mwingine: kila mmoja ni wa pekeeMungu ametufanya tofauti ili tusaidiane.

 

Kila mmoja anahitaji wengine, na kila mmoja ni muhimu kwa mwenzake na Katika maisha ya jamii kuna sehemu ambayo yeye tu anaweza kuijaza.

Wazo hilo linaweza kumsaidia kijana ambaye ni mwepesi kukata tamaa na kujitupa

Daima uhai ni zawadi nzuri kwa mhusika na kwa wenzake wote. Kijana ni zawadi yenye nguvu na wema hata kwa taifa, kiasi kwamba kujali ustawi wa kijana ni kujenga taifa

 KUJIKUBALI

Daima ni muhimu tukubali hali ilivyo, halafu tujitahidi kuifanya bora zaidi. Tusipojikubali kwanza tutahangaika tu hata kukata tamaa. vijana  wanashindwa  kujikubali  jinsi tulivyo.

 

Pengine wanaficha silika zao wasitambulikane na watu, hata wakashindwa kujielewa, wakapatwa na vilema vya ukuaji.

 

Ni lazima waache kujifunika uso kwa vinyago hivyo; badala yake wakabili ukweli wao, wenye sifa na kasoro.

 

Hivyo tu watapitia vizuri mabadiliko ya ujana upande wa mwili, nafsi, jamiimaadili na roho. Hatimaye watakomaa na kushika nafasi yao maishani.

 

Kwa kila mtu ni muhimu kuwa na marafiki; hasa kijana anahitaji kikundi. Lakini hiyo isiwe njia ya kukwepa nafsi yake mwenyewe wala ya kuficha tabia yake kwa kuzungumza, kutembea au kutenda namna fulani wanavyofanya wenzake.

 Kwa hiyo asijifananishe nao. Kila mtu anakua kwa namna yake, akibadilika kwa kiasi tofauti na muda tofauti.

 

Ni lazima ajifunze kuyapokea mabadiliko hayo pia yanayomfanya  kuwa kigeugeu sana, hasa msichana katika mzunguko wake wa kila mwezi: mara anaonekana jasiri au mkorofi, mara amejaa wasiwasi

 

KUJISTAWISHA

Uhai unasukuma kiumbe chochote kistawi, Mimea inakua namna yake, wanyama namna yao, na binadamu polepole zaidi kwa kuwa ndiye kiumbe bora anayehitaji kukomaa pande zake zote

Kulingana na haja yetu ya kukomaa hivyo, sio tu kufikia umri au kimo fulani, ndani mwetu zimo nguvu zinazotuhimiza tujilinde ili tuzidi kuishi wenyewe, tuendeleze uhai tulionao kwa kuzaa, tujitegemee (yaani tumiliki maisha yetu), tutawale vitu na watu ili mambo yaende tunavyotaka

 

Haja iliyoota mizizi mirefu ndani mwetu ni ile ya kujikamilisha tusiwe watu wanaoishi ili mradi tu. Kadiri tunavyokua tunajisikia kuwajibika. Haja hizo zinafanya tujiwekee pia malengo katika utendaji

 

Basi, baada ya kujifahamu, kila mmoja wetu achague na kuazimia awe bora vipi, kwa sababu wenyewe tunaamua tuweje.

Ni wajibu wetu kujipenda na kwa hiyo kujitunza na kujistawisha kimwili, kinafsi, kijamii, kimaadili na kiroho. Kazi hiyo inahitaji nia na bidii za kudumu

Tufuate taratibu za kulinda afya ya mwili, heshima ya mavaziusafi wa mazingira. Tujiepushe na uvivu unaosababisha mawazo na matendo mabaya

 

Tujihadhari na maandishi, picha na maneno yasiyofaa, yasije yakatupotosha kimawazo au kusisimuai. Tuhusiane vema na wengine (adabu, lugha nzuri n.k.). Hasa tufuate dhamiri na kustawisha roho iliyo sehemu bora ya utu wetu ambamo tunashirikiana na Mungu. 

 www.mzunguko.com

 

 

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon