Tuzo ya Ujerumani na Afrika yaenda Tanzania na Madagascar

Tuzo ya Ujerumani na Afrika mwaka huu imewaendea wanaharakati wawili kutoka barani Afrika. Gerald Bigurube kutoka Tanzania na Clovis Razafimalala kutoka Madagascar wamepata kwa pamoja tuzo hiyo inayotolewa kila mwaka.

kwanini tuzo hiyo imetolewa kwa wanaharakati wa ulinzi wa mazingira.

Mkuu wa jopo la majaji kwa ajili ya tuzo hiyo Volker Faigle ameweka wazi wakati wa hotuba yake, kwamba mwanamfalme wa Uingereza wiki chache zilizopita alipokuwa akifungua mkutano wa kimataifa alitoa wito wa kuzuia kwa matumizi ya kupindukia ya ardhi ili kuzuia athari za mabadiliko ya tabia nchi.

Wanaharakati wawili Gerald Bigurube wa Tanzania (kushoto) na Clovis Razafimalala wa Madagascar (kulia) wakiwa pamoja na jopo la majaji pamoja na viongozi wa serikali ya Ujerumani

Ni wito muhimu kama anavyoeleza rais wa majaji Volker Faigle waliowachagua wanaharakati hao wawili wa kulinda mazingira kutoka Afrika

Kuanzia mwaka 1993 wakfu wa Ujerumani na Afrika umejionesha kuwa unapigania amani , demokrasia na maendeleo endelevu.

Rais wa bunge la Ujerumani Wolfgang Schaueble ameeleza kuhusu umuhimu wa bara la Afrika kwa Ulaya.

Amesema hali ya baadaye ya bara la Ulaya itaamuliwa kupitia ushirikiano wa pamoja wa maendeleo zaidi ya bara la Afrika.

Bigurube mwenye umri wa miaka 66 amekuwa tangu miaka 40 iliyopita ni mwanaharakati wa ulinzi wa mazingira nchini Tanzania, ambaye amehusika zaidi katika eneo maarufu duniani la mbuga ya Serengeti.

Kwanza alikuwa mkuu wa shirika la taifa la hifadhi ya wanyamapori la TANAPA, na hivi sasa ni mkurugenzi wa jamii ya maeneo ya zoo mjini Frankfurt.

Jaji wa tuzo hiyo Faigle anamsifu kuwa ni mjenga muhimu wa daraja.

Bigurube anasimama kwa ajili ya ulinzi endelevu wa mazingira, ambayo yanakwenda kwa pamoja na mahitaji muhimu ya jamii na maendeleo.

Gerald Bigurube

www.mzunguko.com


Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu