Mwandishi Phocus Ndayizera azuiliwa Rwanda na kudaiwa kujihusisha na ugaidi

Mwandishi wa habari wa kujitegemea Phocus Ndayizera ameonyeshwa mbele ya vyombo vya habari na polisi wa upelelezi nchini Rwanda wiki moja baada kutoweka

Msemaji wa idara ya polisi ya upelelezi nchini humo amesema kwamba mwandishi huyo anatuhumiwa kwa makosa ya ugaidi.

Mwandishi huyo alifanyia kazi vyombo vya habari mbali mbali na mara kwa mara amekuwa akiripotia BBC, Idhaa ya Kinyarwanda na Kirundi yeye amesema kwamba hajui kwa nini anazuiliwa.

Mwandishi wa BBC aliyeko Kigali, Yves Bucyana, amesema Phocus Ndayizera wakati alipoonekana mbele ya waandishi wa habari kwenye makao makuu ya idara ya polisi inayohusika na upelelezi alikuwa amevalishwa pingu na hali yake ilionesha alikuwa mchovu.

Alipotakiwa na polisi kuwambia waandishi wa habari tuhuma dhidi yake, Bwa Ndayizera amesema kwamba hana habari yoyote kuhusu mashitaka dhidi yake akisisitiza tu kwamba na yeye anasubiri upelelezi kukamilika.

Amesema kwamba alikamatwa katika mtaa wa Nyamirambo jijini Kigali alipokwenda kumuona jamaa yake na kupelekwa sehemu isiyojulikana kabla ya kujikuta katika mahabusu ya polisi kituo cha Remera

Msemaji wa idara ya upelelezi Modeste Mbabazi amewambia waandishi wa habari kwamba Ndayizera anatuhumiwa kwa kujihusha na ugaidi na pia kukutwa na vifaa vya vilipuzi

hatahivyo Polisi wa upelelezi wamekiri kuwa ndio waliokuwa wanamshikilia mwandishi huyo kwa wiki nzima.

Msemaji wa Polisi amesema walisubiri siku kadhaa kutangaza kumshikilia mwandishi huyo kutokana na kwamba makosa ya ugaidi yanafwatiliwa kwa njia ya kipekee tofauti na makosa mengine.

Haijafahamika ni lini mwandishi huyo na wengine wanaotuhumiwa pamoja watakapofikishwa mahakamani

www.mzunguko.com


Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu