Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Tuzo ya Ujerumani na Afrika yaenda Tanzania na Madagascar

November 29, 2018

Tuzo ya Ujerumani na Afrika mwaka huu imewaendea wanaharakati wawili kutoka barani Afrika. Gerald Bigurube kutoka Tanzania na Clovis  Razafimalala kutoka Madagascar wamepata kwa pamoja tuzo hiyo inayotolewa kila mwaka.

 kwanini  tuzo  hiyo imetolewa  kwa  wanaharakati  wa  ulinzi  wa  mazingira.

 

Mkuu  wa  jopo la  majaji  kwa  ajili  ya  tuzo  hiyo Volker Faigle  ameweka  wazi  wakati wa  hotuba  yake, kwamba  mwanamfalme  wa  Uingereza  wiki  chache zilizopita  alipokuwa  akifungua  mkutano wa  kimataifa  alitoa  wito  wa kuzuia kwa  matumizi  ya  kupindukia  ya  ardhi  ili  kuzuia athari za mabadiliko  ya  tabia  nchi. 

Wanaharakati wawili Gerald Bigurube wa Tanzania (kushoto) na Clovis Razafimalala wa Madagascar (kulia) wakiwa pamoja na jopo la majaji pamoja na viongozi wa serikali ya Ujerumani

 

Ni  wito  muhimu  kama  anavyoeleza  rais  wa  majaji  Volker  Faigle waliowachagua wanaharakati  hao  wawili  wa   kulinda  mazingira kutoka  Afrika

 

Kuanzia  mwaka  1993  wakfu  wa  Ujerumani  na  Afrika  umejionesha kuwa  unapigania  amani , demokrasia  na  maendeleo  endelevu.

 

Rais wa  bunge  la  Ujerumani  Wolfgang Schaueble ameeleza  kuhusu umuhimu  wa  bara  la  Afrika  kwa  Ulaya.

 

Amesema  hali  ya  baadaye ya  bara  la  Ulaya  itaamuliwa  kupitia  ushirikiano  wa  pamoja  wa maendeleo  zaidi ya  bara  la  Afrika.

Bigurube  mwenye  umri  wa  miaka  66 amekuwa  tangu  miaka  40 iliyopita  ni  mwanaharakati  wa  ulinzi  wa  mazingira  nchini  Tanzania, ambaye  amehusika  zaidi  katika  eneo  maarufu  duniani  la   mbuga ya  Serengeti.

Kwanza  alikuwa  mkuu  wa  shirika  la  taifa  la  hifadhi ya  wanyamapori  la  TANAPA, na  hivi  sasa  ni  mkurugenzi  wa  jamii ya  maeneo  ya  zoo  mjini  Frankfurt.

 

Jaji  wa  tuzo  hiyo Faigle  anamsifu  kuwa  ni  mjenga  muhimu  wa daraja.

 

Bigurube  anasimama  kwa  ajili  ya  ulinzi  endelevu  wa mazingira, ambayo  yanakwenda  kwa  pamoja  na  mahitaji  muhimu  ya jamii  na  maendeleo.

 

Gerald Bigurube

 

www.mzunguko.com

 

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload