Mnamo mwaka wa 1821 nchi ya Panama inapata Uhuru kutoka Hispania ikiwa sehemu ya nchi ya kolombia

[siku kama ya leo tarehe 28 mwezi wa 11 mwaka wa 1821 nchi ya Panama inapata uhuru]

Panama ni nchi ya mwisho kusini mwa Amerika ya Kati. Shingo ya nchi ya Panama hutazamwa kuwa mpaka kati ya bara la Amerika ya Kaskazini na lile la Amerika ya Kusini

Panama Imepakana na Kosta Rika na Kolombia; pwani ya Bahari ya Karibiiko upande wa kaskazini na pwani ya Pasifiki upande wa kusini.g

Nchi iko kwenye sehemu nyembamba kabisa ya Amerika ya Kati.

Mfereji wa Panama hukata shingo ya nchi na kufanya jina la Panama kujulikana kote duniani

Baada ya ukoloni wa Hispania Panama ilikuwa sehemu ya kaskazini ya Kolombia. Majaribio mbalimbali ya uasi dhidi ya Kolombia kwa shabaha ya kuwa nchi ya pekee katika karne ya 19 hayakufaulu

Mabadiliko makubwa yalikuja na ujenzi wa mfereji wa Panama

SIMON BOLIVAR

Simon Bolivar alikuwa mwanasiasa na mwanajeshi katika Amerika ya Kusini aliyeongoza mapambano dhidi ya ukoloni wa Hispania. Nchi mbalimbali humkumbuka kama baba wa taifa lao

Alizaliwa 24 Julai 1783 mjini Caracas (wakati ule: Granada mpya, leo: Venezuela) akaaga dunia mjini Santa Marta (Kolombia) tar. 17 Desemba 1830.

Kama jemadari alishinda jeshi la Hispania kati ya 1810 na 1820.

Mfereji wa Panama

www.mzunguko.com


Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu