Tetesi za Soka Ulaya Jumatano 28.11.2018; Cole, Wenger, Fabinho, Dembele, Steffen, Pochettino

November 28, 2018

 Beki wa zamani wa England Ashley Cole, 37, amepewa ofa mpya na klabu ya LA Galaxy - siku chache baada ya kuachiliwa na klabu. (Sun)

 

Lakini mlinzi huyo wa zamani wa Arsenal na Chelsea anataka kurejea kwenye kandanda ya Uingereza na amepata ofa kutoka vilabu kadhaa. Mirror

 

Paris St-Germain watatumia mechi yao na Liverpool kufungua mazungumzo kuhusu kumwendea mlinzi raia wa Brazil Fabinho, 25. (L'Equipe - in French)

 

Kipa wa PSG Gianluigi Buffon anaamini washambuliaji watatu wa Liverpool - Mohamed Salah, Sadio Mane na Roberto Firmino - ndio bora zaidi dunaini. (Mirror)

 

Mshambuliaji Mfaransa Ousmane Dembele, 21, amewaambia Barcelona kuwa hataki kuondoka klabuni mwezi Januari. (ESPN)

Manchester City wanakaribia kufikia makubaliano na Columbus Crew na kipa wa Marekani Zack Steffen, 21. (Sky Sports)

 

Meneja wa Tottenham Mauricio Pochettino anataka kusimamia klabu ya Sirie A nchini Italia. (Standard)

 

Meneja wa Manchester United Jose Mourinho anamlenga beki wa Porto mwenye miaka 20 raia wa Brazil Eder Militao. (Daily Record).

Mshambulji wa zamani wa Ivory Coast Didier Drogba, 40, anasema alijifunza sana kutoka kwa mchezaji mwenake wa zamani huko Chelsea na meneja wa Derby Frank Lampard, 40. (Goal)

 

www.mzunguko.com

 

 

 

 

 

 

 

 

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon