Je wajua nchi iliyowahi kuwa kati ya nchi tajiri zaidi afrika lakini tangu mwaka 2002 uchumi na hali

Cote d'Ivoire ( kifaransa inatamkwa; kot divwar;

kiswahili inatamkwa "Pwani la pembe za ndovu" au Kodivaa,

na kwa kiingereza inatamkwa Ivory Coast.

Ivory Coast ni nchi ya Afrika ya Magharibi. Imepakana na Liberia na Guinea upande wa magharibi, Mali na Burkina Faso kaskazini, Ghana kwenye mashariki na Ghuba ya Guinea ya Atlantiki upande wa kusini.

Nchi ya ivory coast Iliwahi kuwa kati ya nchi tajiri zaidi za Afrika lakini tangu mwaka 2002 uchumi na hali ya maisha zimeharibika kutokana na vita ya wenyewe kwa wenyewe.

Serikali ya Côte d'Ivoire (Ivory Coast)inachukua nafasi katika mfumo wa uwakilishi wa uraisi katika jamhuri ya kidemokrasia,

ambapo Rais wa Cote d'Ivoire ni mkuu wa nchi na vilevile ni kiongozi wa serikali, na inafuata mfumo wa vyama vingi.

Nguvu ya kiutendaji hutimizwa na serikali tu. Suala la utunzi wa sheria hutekelezwa kwa njia ya serikali yenyewe au bunge.

Mji mkuu rasmi tangu 1983 ni Yamoussoukro; hata hivyo, Abidjan unabaki kuwa kitovu cha utawala.

Nchi nyingi huweka balozi zao mjini Abidjan, ijapokuwa baadhi yao (ikiwa ni pamoja na Uingereza) wamefunga harakati zao kwa sababu ya fujo zinaoendelea na ushambuliaji dhidi ya Wazungu.

Wakazi wanaendelea kupata shida kwa kufuatia vita ya wenyewe kwa wenyewe inayoendelea.

www.mzunguko.com


Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu