Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Wachina 'wameunda' binadamu asiyeweza kuambukizwa Ukimwi?

November 27, 2018

Mwanasayansi kutoka Uchina ambaye amedai kuwa amesaidia kuzalisha watoto wa kwanza ambao chembe zao za jeni zilihaririwa kabla ya kuzaliwa na kwamba hawawezi kuambukizwa Ukimwi, ameshutumiwa vikali na madai yake kutiliwa shaka.

Prof He Jiankui anadai kwamba wasichana hao pacha, waliozaliwa wiki chache zilizopita, vinasaba vyao (DNA) vilifanyiwa ukarabati wakiwa bado ni viinitete kuwawezesha kutoambukizwa Virusi Vinavyosababisha Ukimwi (VVU)

 

Madai yao aliyoyatoa kwenye kanda ya video iliyosambazwa na shirika la habari la Associated Press hayajapigwa darubini na yamewaghadhabisha wanasayansi wengine.

 

Wamesema wazo hilo lenyewe ni la kuogofya.

Kazi kama hizo za kisayansi, za kuhariri jeni za binadamu, zimepigwa marufuku katika mataifa mengi

 

Vizazi vijavyo

Wanasayansi wanaamini kwamba uhariri wa jeni unaweza kuwaepushia watu magonjwa ya urithi yanayotokana na vinasaba, kwa kufuta chembe za jeni zinazosababisha magonjwa hayo au hata kuzifanyia ukarabati mtoto akiwa bado ni kiinitete

 

Lakini wataalamu wana wasiwasi kwamba kuhaririwa huko kwa jeni kunaweza kusababisha madhara makubwa sio tu kwa mtoto mwenyewe bali pia vizazi vya baadaye ambavyo vitayarithi marekebisho yaliyofanywa na wanasayansi kwenye vinasaba.

Katika mataifa mengi, ikiwemo Uingereza, kuna sheria zinazoharamisha kuhaririwa kwa jeni hata katika mchakato wa kuwasaidia binadamu kutungisha mimba.

 Wanasayansi wanaweza kufanya utafiti kuhusu uhariri wa jeni kwa kutumia viinitete vilivyotupwa baada ya mwanamke kutungishwa mimba kwenye maabara, shughuli inayofahamika kama IVF, lakini hilo huruhusiwa tu kwa sharti kwamba viinitete hivyo vitaharibiwa baada ya utafiti na visitumiwe kuzalisha mtoto.

 

Watoto wa maabara'

Lakini Prof He, aliyesomea Stanford nchini Marekani na anayefanyia kazi yake katika maabara moja katika jiji la Shenzhen kusini mwa China anasema alitumia vifaa vya kuhariri jeni 'kuwaunda' watoto hao wawili pacha waliopewa majina "Lulu" na "Nana".

Kwenye video, amedai kwamba alifanikiwa kuondoa jeni kwa jina CCR5 kwenye viinitete vya na kuwawezesha watoto hao kuwa na kinga ya kudumu dhidi ya Ukimwi hata wakikumbana na virusi hivyo.

 

www.mzunguko.com

 

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload