Tetesi za Soka Ulaya Jumatatu 26.11.2018: Dembele, Gomes, Hazard, Fabregas, Rice, Alba


Mshambuliaji Mfaransa Ousmane Dembele, 21, ameomba kuondoka Barcelona mwezi Januari na kuondoka kwake kutamruhusu Neymar kurudi Nou Camp kutoka Paris St-Germain. (Goal)

Mshambuliaji wa Chelsea Eden Hazard, 27 amekana kuwa atahamia Paris St-Germain, lakini amekiri kuwa ataondoka Stamford Bridge msimu huu. (Canal+ via Goal)

Mkurugenzi wa Milan Leonardo ameripotiwa kuwa kwenye mazungumzo na Chelsea kuhusu kiungo wa kati Cesc Fabregas, 31, na walinzi Gary Cahill, 32, na Andreas Christensen, 22. (Football Italia]

Manchester United ilituma maajenti kumtazama kijana mlinzi wa West Ham Declan Rice, 19, wakati Hammers walishindwa kwa mabao 4-0 na Manchester City siku ya Jumamosi. (Metro)

Beki wa Barcelona Jordi Alba, 29, amekiri kuwa hajapewa mkataba mpya klabuni na kuacha hatma yake gizani. (ESPN)

Manchester United wanaweza kungoja kumsaini kiungo wa kati wa Roma Lorenzo Pellegrini baada ya kugundua kuwa kupengee cha kuuvunja mkataba wake kinaweza kutumiwa mwisho wa msimu. (Mirror via Manchester Evening News]

Meneja wa Newcastle Rafa Benitez anasema hataki kurejea kwa Serie A siku za usoni ikiwa ndoto yake haitatimia huko St James' Park. (Newcastle Chronicle)

www.mzunguko.com


Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu