Je wajua Ziwa Turkana ndio ziwa kuu katika jangwa ulimwenguni?


Ziwa Turkana ni ziwa lililopo kaskazini mwa Kenya. Halina mto unaotoka, hivyo maji yanayoingia yanapotea kwa njia ya uvukizaji. Ni ziwa kubwa la Kenya lakini linapatikana kaskazini ndani ya Ethiopia.

Ni ziwa la jangwani ambalo ni kubwa kuliko yote duniani.

Umbo la ziwa ni kama kanda ndefu linaloelea kutoka kaskazini kwenda kusini.

Urefu wa ziwa ni kilomita 290, upana wake hadi kilomita 32. Eneo la maji ni km² 6,405. Ndani ya ziwa kuna visiwa vitatu vidogo vinyavoitwa Kisiwa cha kusini, cha kati na cha kaskazini

Ziwa Turkana linavyoonekana kutoka angani

Wenyeji wametumia majina mbalimbali kufuatana na lugha zao. Waturkana hutumia "anam Ka'alakol" yaani "ziwa la samaki wengi".

Wapelelezi Wazungu wa karne ya 19 walisikia jina la "Basso Narok" ingawa haieleweki hii ilikuwa lugha gani.

Kimataifa jina lilijulikana kwa jina la "Ziwa Rudolph" (Rudolfsee, Lake Rudolph) lililotolewa na mpelelezi Mhungaria Sámuel Teleki kwa heshima ya mtemi Rudolph, mtoto wa mfalme wa Austria-Hungaria

www.mzunguko.com


Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu