Je wajua undani wa Hifadhi ya kisiwa cha Saanane kilichopo mkoani Mwanza

Kisiwa cha Saanane (Saanane Island National Park) ni hifadhi ya taifa la Tanzania na ni hifadhi ndogo yenye eneo la kilomita za mraba 2.18, na iko umbali wa kilometa 2 kusini magharibi kutoka katikati ya jiji la Mwanza, katika Ghuba ya Ziwa Victoria nchini Tanzania.

Hifadhi hii ilianzishwa kama bustani ya kwanza ya wanyama nchini Tanzania mwaka 1964 ikawa hifadhi kamili mwaka 2013

Lengo la kuanzishwa kwake ilikuwa kuhamasisha uhifadhi wa wanyama na kuelimisha jamii, pamoja na kutoa nafasi kwa wakazi wa Mwanza kupumzika.

Jina la hifadhi hii lilitokana na muanzilishi wa bustani aitwaye Saanane Chawandi. Kati ya mwaka 1964 na 1966 wanyama mbalimbali walihamishiwa katika kisiwa hiki.

Wanyama hao ni pamoja na mbogo, digidigi, tembo, pofu, pongo, swala pala, ngiri, pundamilia, kima, twiga, nungunungu, mamba n.k

Wanayama wakali kama faru na mbogo walifungiwa na wanyama wapole waliachwa huru

picha ya kifaru

picha ya mbogo

Bustani hii iliachwa kuwa pori la akiba mwaka 1991

Muonekano wa Ziwa Victoria katika kisiwa cha Saanane ni kivutio kikubwa. Vilevile muonekano wa Kisiwa cha Saanane uwapo Mwanza ni kivutio kingine kikubwa

Hifadhi hii inafikika wakati wowote katika mwaka. Na unaweza kufika kwa kutumia boti ukitokea katika mji wa Mwanza.

www.mzunguko.com


Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu