Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Watu 26 wafariki kwenye ajali ya mashua ziwa Victoria Uganda

November 25, 2018

Polisi nchini Uganda wanasema kuwa watu 26 wamefariki kufuatia ajali ya mashua iliyotokea ziwa Victoria.

Shughuli za uokoaji zinaendela lakini naibu Inspekta mkuu wa polisi anayesimamia oparesheni hiyo Asuman Mugenyi anasema kuna uwezekano mdogo wa kupata manusura

Anasema mashua hiyo ilikuwa inasafirisha zaidi ya watu 90 kwenda kisiwa kimoja katika ziwa Victoria

 

Mashua hiyo iliyokuwa na watu waliokuwa wanaelekea sherehe, ilipata ajali katika kaunti ndogo ya Mpatta wilaya ya Mukono

 

Prince David Wasajja, ndugu wa mfalme wa Buganda mfalme Kabaka Ronald Mutebi alikuwa pia kwenye mashua hiyo lakini aliokolewa,

 www.mzunguko.com

 

 

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload