Rais wa zamani wa Zimbabwe Robert Mugabe ' yupo katika hali mbaya ashindwa ata kutembea,kwa mujibu wa Rais Emmerson Mnangagwa wa zimbabwe

November 25, 2018

Rais wa zamani wa Zimbabwe Robert Mugabe mwenye umri wa miaka 94, anaripotiwa kuwa katika hali mbaya ya kiafya kiasi ya kwamba hawezi tena kutembea.

 Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangangwa amewaambia wafuasi wa chama tawala, kwamba Mugabe amekuwa hospitali nchini Singapore kwa miezi miwili anakopatia matibabu.

 Katika taarifa yake hiyo ya jana, Mnangagwa amesema Mugabe alipanga kurudi Zimbabwe Oktoba 15 lakini kutoka na hali hali yake bado kuwa mbaya anatarajiwa kurudi Novemba 30.

Mnangagwa hakutoa taarifa zaidi juu ya afya ya kiongozi huyo wa zamani.

 

Mugabe alikuwa kiongozi mzee zaidi duniani kabla ya kuondoshwa madarakani baada ya kuiongoza Zimbabwe kwa miaka 37.

 www.mzunguko.com

 

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon