Je wajua kwamba Kimondo cha Mbozi ni jiwe kubwa kutoka anga la nje linaloweza kuangaliwa huko Mbozi

November 24, 2018

Kimondo cha Mbozi ni kimondo ambacho kimeanguka kutoka angani karibu na mji wa Vwawa. Kinakadiriwa kuwa na uzito wa takriban tani 16, kilianguka katika kilima cha Mlenjewilayani Mbozi katika mkoa wa Mbeya, Tanzania

Kipo kati ya vimondo vizito 10 vinavyojulikana duniani. Kina urefu wa mita 3.3, upana wa mita 1.63 na kimo cha mita 1.22

Kina maumbile maalum tofauti na vimondo vingine vinavyopatikana ulimwenguni kwa kuwa hiki ni hasa cha chuma. Chuma ni 90.45%, nikeli 8,69%sulfuri 0,01% na fosfori 0,11% ya masi yake. Ndani yake vipande vidogo vya silikati vinapatikana

Wenyeji wa eneo walijua kimondo hiki tangu muda mrefu; kilielezwa kisayansi mara ya kwanza mwaka 1930 na wakati ule hapakuwa na dalili za kasoko;

 

kwa hiyo inawezekana ya kwamba ama kilifika kwenye uso wa Dunia kwa pembe butu sana na kuvingirika hadi kukaa au muda wa kugonga uso wa dunia ni mrefu sana hadi dalili zote za kasoko asilia zilipotea tayari kutokana na mmomonyoko

 

KASOKO

Kasoko ni shimo kwenye ardhi kutokana na mlipuko au mshtuko wa kugongwa na gimba

 

Kuna aina mbalimbali za kasoko

 • kasoko ya mlipuko, kwa mfano wa bomu iliyolipuka ndani ya ardhi au juu ya uso wa ardhi

 • kasoko ya dharuba (mgongano) kutokana na kugongwa kwa uso la gimba na gimba nyingine, kwa mfano kama Dunia, sayari nyingine au Mwezi imegongwa na meteoridi au asteroid

 • Kasoko ya volkeno: shimo ambako zaha (lava) inatoka nje

 • Kasoko ya Tycho mwezini kutokana na dharuba ya kimondo

 • Kasoko huko Arizona(Marekani) kutokana na mgongano wa kimondo

 • Kasoko kutokana na milipuko ya bomu za kinyuklia chini ya ardhi kwenye eneo la jaribio la Marekani huko Nevada.

 •  

  www.mzunguko.com

   

   

   

   

   

 

 

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload

Tufuate kupitia:
 • YouTube Social Icon
 • Twitter Social Icon
 • Black Instagram Icon
 • Facebook Social Icon