Je wajua kwamba Hifadhi ya Ngorongoro imepokelewa katika orodha ya urithi wa dunia ya UNESCO?

Ngorongoro ni eneo kubwa nchini Tanzania, lenye umbali wa takriban kilomita 180 kutoka Arusha; pia ni hifadhi ya taifa inayojulikana kote duniani.

Kuna jumla ya wanyamapori wakubwa takriban 25,000, wakiwa pamoja na vifaru, viboko, nyumbu, pundamilia, nyati, simba, fisi na chui.

Bidii kubwa zaidi ya kulinda wanyama aina ya vifaru zinahitajika haraka kwa sababu idadi ya wanyama hao inazidi kupungua

Mabaki ya zamadamu katika Olduvai Gorge yanaonyesha kwamba wanyama hao waliokoma walikuweko tangu miaka milioni 3 iliyopita

Mwaka 1979 Ngorongoro ilipokewa katika orodha ya Urithi wa Dunia ya UNESCO upande wa uasilia.

UNESCO

UNESCO ni kifupisho cha United Nations Educational, Scientific and Cultural Organization yaani Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa.

Ni kitengo cha Umoja wa Mataifa ambacho kinashughulika habari za elimu, sayansi na utamaduni duniani.

Kisheria UNESCO ni shirika la kujitegemea lenye madola ya wanachama 191.

Kati ya shughuli muhimu za UNESCO mojawapo ni Orodha ya Urithi wa Dunia inayojumlisha mahali penye umuhimu wa pekee kihistoria, kisayansi au kiutamaduni.

Katika sekta ya utalii, ambayo nchi ya Tanzania huitegemea, ni muhimu serikali iandae miundombinu, hasa barabara zenye ubora wa hali ya juu, ili zitumike kwa muda mrefu na kuboresha sekta nyingine.

www.mzunguko.com


Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu