Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Rais wa Marekani Donard Trump apingana na CIA kuhusu mauaji ya khashoggi

November 22, 2018

Trump asema CIA haijamlaumu bin Salman kuamuru mauaji ya mwanahabari khashoggi.

Rais wa Marekani Donald Trump amesema shirika la ujasusi la nchi hiyo CIA halijahitimisha uchunguzi wake kwa kumlaumu mwanamfalme wa Saudi Arabia Mohammed bin Salman kuamuru mauaji ya mwanahabari Jamal Khashoggi

Khashoggi aliuawa Oktoba 2 ndani ya ubalozi mdogo wa Saudia jijini Istanbul, Uturuki.

Wakati wa uhai wake alikuwa mkosoaji mkubwa sera za Saudia hususani mwanamfalme bin Salman. Alikimbilia Marekani mwaka 2017 akihofia usalama wake.

 

Maafisa wa CIA waliviambia vyombo vya habari vya Marekani kuwa operesheni ya kumuua Khashoggi lazima ilihitaji ruhusa ya bin Salman ili kufanikishwa.

Hata hivyo mamlaka za Saudia zinasisitiza kuwa operesheni hiyo ilikuwa haramu na bin Salman hakuwa na ufahamu wowote wa kutokea kwake.

.(CIA) Hawakuhitimisha hivyo," Trump alijibu hivyo mara baada ya kuulizwa kuhusu ripoti ya CIA juu ya mauaji ya Khashoggi

Kauli hiyo ya Trump ameitoa jana Alhamisi wakati ambapo bin Salman ameanza ziara ya kikazi nje ya nchi yake toka Khashoggi alipouawa.

Kwa sasa yupo katika nchi ya Falme za Kiarabu (UAE) ambayo ni mshirika mkubwa wa Saudia ndani ya kanda ya Mashariki ya Kati.

Bin Salman pia anatarajiwa kuiwakilisha nchi yake katika mkutano wamataifa 20 yenye nguvu kubwa kiuchumi duniani, G20, utakaofanyika mwisho wa mwezi jijini Buenos Aires, Argentina. Ukiachana na bin Salman na Trump,

mkutano huo utahudhuriwa pia na viongozi kutoka Uturuki na nchi nyingine za magharibi amabazo zimekuwa zikiishinikiza Saudia kueleza ukweli mtupu kuhusu sakata la Khashoggi..

 Wakati huohuo, Ufaransa imetangaza kuwawekea vikwazo raia 18 wa Saudia ambao wanashukiwa kutekeleza mauaji hayo. Watu hao pia wameshawekewa vikwazo na Marekani, Uingereza na Ujerumani.

Hata hivyo, bin Salman hayupo kwenye listi hiyo, msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Ufaransa amethibitisha

 

 www.mzunguko.com

 

 

 

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload