Mwaka wa 1987 tarehe 22 mwezi wa 11 Mike Tyson alivunja rekodi katika historia ya mchezo wa masumbwi kwa kuwa kijana mdogo mwenye uzito wa juu akiwa na umri wa miaka 20

November 22, 2018

 Michael Gerard Tyson (amezaliwa 30 Juni 1966) ni mpiga ngumi wa uzito wa juu duniani unaotambuliwa na Shirikisho la Ngumi Duniani (WBC).

 Ni bondia wa kwanza kuwahi kutwaa taji hilo akiwa na umri mdogo.

Mike alizaliwa katika mji wa Brooklyn New York. Alikuwa mtoto mtukutu akijihusisha na matukio ya uporaji mitaani.

Alipelekwa katika shule ya kurekebisha tabia (Jela ya watoto) huko New York.

 Akiwa huko alionekana mwenye kipaji na mwalimu wa ngumi Mmarekani aitwaye Cus D'Amato ambaye matunda yake mengine ni mwanamasumbwi aitwaye Floyd Petterson na kutwaa taji la ngumi 1956.

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon