Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Mwaka 2005 Dr Angel merkel alikuwa mwanamke wa kwanza kuwa chansela wa ujerumani

November 22, 2018

[siku kama ya leo tarehe 22 mwezi wa 11 mwaka 2005 Dr angel  alikuwa mwanamke wa kwanza kuwa  chansela wa ujerumani]

Dk. Angela Dorothea Merkel  amezaliwa tar. 17 Julai 1954, mjini Hamburg ni mwanafizikia na mwanasiasa wa Kijerumani, na ni Chansela wa Ujerumani tangu 22 Novemba 2005.

 alizaliwa 1954 mjini Hamburg katika familia ya Horst na Herlind Kasner.

Babake alikuwa mchungaji wa Kanisa la Kiluteri, mama alikuwa mwalimu.

 

Mwaka uleule familia ilihamia Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kijerumani (ambayo ilikuwa Ujerumani ya Mashariki,

 

kabla ya Ujerumani zote mbili kuungana na kuwa moja) ambapo aliishi huko hadi Muungano wa Ujerumani ulipofanyika mnamo mwaka wa 1990.

 

Tangu 1957 familia iliishi mjini Templin katika kaskazini ya nchi ambako mchungaji Kasner alikuwa mkuu wa chuo cha theolojia.

 

Mamake Angela alizuiliwa kufanya kazi ya ualimu kwa sababu serikali ya kikomunisti haikutaka mke wa mchungaji kuwa shuleni. Angela ana wadogo wawili.

 

Alisoma shule ya sekondari kwake Templin alipofaulu hasa katika masomo ya Kirusi na hisabati. Aliingia pia katika Umoja wa Vijana wa Chama cha Kikomunisti FDj 

 

Alipomaliza shule kwenye mwaka 1973 wastani ya maksi zake ilikuwa A+.

1973 hadi 1978 alisoma fizikia kwenye chuo kikuu cha Leipzig.

  Mwaka 1977 alifunga ndoa na mwanafunzi mwenzake Ulrich Merkel lakini ndoa hii ilitalikiwa 1982, ni hapa alipopata jina lake.

Tangu 1978 aliajiriwa kwenye Taasisi Kuu kwa Kemia ya Kifizikia katika Berlin ya Mashariki.

Hapa alimaliza tasnifu ya uzamifu mwaka 1986 iliyokubaliwa kwa heshima kuu "magna cum laude". Aliendelea na kazi kweye taasisi ya kemia ya kichanganuzi.

 

Merkel amekuwa mwanamke wa kwanza kuwa Kansela kunako tar. 22 Novemba 2005 katika serikali ya mseto wa vyama viwili vya kisiasa vya Kijerumani, yaani kati ya CDU/CSU na SPD.

 

www.mzunguko.com

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload