Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Je wajua kwamba Asha-Rose Mtengeti Migiro ni mwanasiasa wa kwanza kutoka nchini Tanzania kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa?

November 23, 2018

 Asha-Rose Mtengeti Migiro  aliwahi kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa. Alipewa cheo hicho na Katibu Mkuu Ban Ki-moon tarehe 5 Januari 2007.

Hadi kuteuliwa kwa cheo cha UM alikuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Tanzania tangu Januari 2006. Wajibu huo alipewa na rais Jakaya Kikwete aliyemteua kumfuata katika wizara ya mambo ya nje iliyoshikwa awali na Kikwete mwenyewe.

Chini ya rais Benjamin Mkapa Migiro alikuwa Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto. Alikuwa mbunge kwa njia ya kiti maalumu cha wanawake.

 

Kabla ya kujiunga na siasa alifundisha kwenye Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Alisoma digrii za bachelor na  kupata master  Dar es Salaam.

 

Mwaka 1992 akaongeza na  udaktari wa sheria kwenye Chuo kikuu cha Konstanz (Ujerumani). Akarudi Tanzania alipoanza kufundisha. Akawa mwanachama wa CCM

Akiwa Mwislamu ameolewa na Cleophas Migiro wana watoto wawili wa kike.

www.mzunguko.com

 

 

 

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload