Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

JE WAJUA MTI ULIYO MUHIMU ZAIDI KIUCHUMI AFRIKA MAGHARIBI

November 22, 2018

Mchikichi  ni kati ya miti iliyo muhimu zaidi kiuchumi duniani. Matunda yake huleta mawese ambayo hutumika sana kama mafuta ya kupikia, pia  kwa ajili ya madawa mbalimbali, na siku hizi  hutumika kama diseli.

 Mchikichi ni kati ya miti iliyo muhimu zaidi kiuchumi. Matunda yake huleta mawese ambayo hutumika sana kama mafuta ya kupikia, pia kwa ajili ya madawa mbalimbali na siku hizi hutumika kama diseli.

 

Mti unakua hadi kimo cha m. 30. Matunda yake ni madogo yakiwa pamoja kwa shingo. Jumla ya mti mmoja Unaweza kufikia 50 KG.

Matunda haya huharibika haraka hivyo ni muhimu kuyashughulika mara moja baada ya mavuno.

 

Asili ya Mchikichi ni Afrika ya Magharibi. Mti huu ulipewa jina la kisayansi "Elaeis guenesis" kwa sababu kiasili ilipatikana kwa wingi katika nchi za kanda ya Guinea.

Siku hizi inakuzwa zaidi katika Amerika na hasa Asia ya kusini.

 ASILI YA MTI WA MCHIKICHIKI.

Kabla ya ukoloni  michikichi ilipatikana katika kanda ya kitropiki ya  Afrika  hasa  katika  kanda  ya Guinea,jamhuri ya kidemokrasia ya kongo, benin,Nigeria, Senegal, sierra leone  na Togo.

 

Lakini kwa  sasa michikichi  pia inapatikana   afrika mashariki, Kenya, Uganda na Tanzania.

 

JE WAJUA MAFUTA YA MAWESE HUTOLEWA KWENYE MTI WA MCHIKICHI

 

Mafuta ya Mawese ni mafuta ya kula yanayotolewa,katika matunda ya mti wa mchikichi ( Elaeis guineensis]. Ni mfuta ya kupikia ya afrika,hasa penye asili ya mchikichi kutokana na kupatikana kwa wingi.

 

Mawese yanatumika kama mafuta ya kupikia  moja kwa moja  Baada yakutolewa na wakulima wenyewe na kuonyesha rangi nyekundu. mawese yanatengenezwa kibiashara kiwandani na  rangi huwa  inaondolewa kwa njia ya kusafisha mafuta kwenye vichujio.

Baada ya kusafishwa huwekwa kwenye makopo au chupa na kuuzwa madukani au kupelekwa nje. Mafuta haya yanatumika pia viwandani kwa kutengeneza sabuni, mishumaa, mafuta ya kupakaa mwilini na aina mbalimbali ya madawa na urembaji.

 

 

JINSI MAWESE YANAVYOWEZA KUTUMIKA KUTENGENEZEA DIZEL

 

Mawese hutumika pia kiteknolojia tangu miaka ya nyuma kwa kutengeneza dizeli. Hasa nchini Malaysia teknolojia hii imesonga mbele.

Malaysia inajaribu kupunguza gharama za kununua petroli na dizeli kwa kutengeneza kiwanda kikubwa cha kusafisha mawese kuwa dizeli

 

Hatahivyo, Sheria ya Malaysia inadai kuanzia mwaka 2007 ya kwamba dizeli yote inayouzwa nchini iwe na 5% dizeli ya mawese.

 

MAWESE KATIKA HISTORIA YA AFRIKA MAGHARIBI

 

Mawese yalikuwa muhimu sana katika uchumi na historia ya Afrika ya Magharibi wakati wa karne ya 19 BK. Ulaya iliingia katika  mapinduzi ya viwanda  ikahitaji mafuta ya kutia grisi kwa ajili ya mashine za viwanda vyake. Mafuta haya yalipatikana katika nchi za Guinea hasa eneo la delta ya Niger.

 

Kiuchumi kwa nchi za Afrika ya Magharibi biashara ya mawese ilichukua nafasi ya biashara ya watumwa; hadi mwanzo wa karne ya 19 falme za pwani zilitajirika kwa kuwauzia wafanyabiashara Wazungu watumwa kwa ajili ya masoko ya Amerika.

Biashara hii ya watumwa ilipigwa marufuku polepole na  Mabadiliko ya sheria katika Uingereza yalitangulia.

 

Mapatano ya kimataifa kwenye Mkutano wa Vienna mwaka 1815 yalipakana na  biashara hii  mpaka ikapungua hadi kwisha.

Umuhimu mpya wa Afrika ya Magharibi kwa ajili ya Ulaya ulikuwa mafuta ya mawese. viini vilipelekwa Ulaya kwa sababu mawese asilia huharibika haraka.

Kabla ya kuwepo kwa viwanda Afrika, viini viliweza kusafirishwa mbali bila kuharibu mafuta ndani yake.

Mawese ya tunda lenyewe huwa  linaharibika kama halitengenezwi kwa kufuata mbinu mbalimbali zinazopatikana kiwandani lakini si rahisi kuzitumia katika uzalishaji wa kienyeji.

ZAO LA MCHIKICHI HULIMWA MKOA GANI HAPA TANZANIA

Zao la mchikichi   hapa Tanzania hulimwa  katika mkoa wa  kigoma,  mkoa  wa mbeya na Tanga kwa kiasi  kidogo mti wa mchikichi hulimwa katika Mikoa ya Kagera,pwani na Rukwa.

 

 Katika kunyenyua uchumi wa taifa letu  serikali ya awamu ya tano imetoa kipaumbele kwa  mkoa wa kigoma kuweza kulima zao la mchikichi  litakalokuwa na manufaa makubwa ikiwemo upatikanaji wa mafuta ya kula, upatikanaji wa  sabuni kupitia zao  la mchikichi. Lakini uchumi wetu    utakuwa kwa kiasi kikubwa kupitia mti wa mchikichi.

 

www.mzunguko.com

 

 

 

 

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload