Nedim Yasar: Jambazi sugu auawa baada ya kustaafu na kuandika kitabu Denmark


Aliyekuwa kiongozi wa kundi la wahalifu ambaye aliandika kitabu kuhusu jinsi aliishi maisha yake, ameuawa kwa kupigwa risasi siku moja kabla ya kutolewa kitabu chake.

Nedim Yasar, 31, alipigwa rasasi wakati akitoka kuzindua kitabu hicho siku ya Jumatatu kwenye mji mkuu wa Copenhagen.

Yasar alipelekwa hospitalini lakini akafariki kutokana na majeraha. Kitabu chake kilichapishwa siku ya Jumanne.

Awali alikuwa amesema kulikuwa na njama ya kumuua mwaka uliopita.

Katika kisa hicho cha siku ya Jumatatu mtu ambaye alikuwa amevaa vazi leusi alimfyatulia Yasar takriban risasi mbili kwa mujibu wa polisi wa Copenhagen

kwa mujibu wa polisi Yasar, ambaye alizaliwa nchini Uturuki na kuwasili Denmark akiwa na umri wa miaka minne, alikuwa kiongozi wa genge la wahalifu la mjini Copenhagen, Los Guerreros, kundi sugu lenye uhusiano na biashara za dawa za kulevya.

Alihama genge hilo mwaka 2012 na kujiunga na mpango wa kubadili tabia baada ya kugundua kuwa angekuwa baba kulingana na shirika la habari la Ritzau

Kisha akawa mshauri wa vijana na kujitengenezea jina kwa kuandaa kipindi kwenye kituo cha radio cha Radio24syv.

Kufuatia kufichuka kwa taarifa za kuuliwa kwa Yasar, Radio hiyo ilichapisha picha ya ofisi yake ikiwa na bendera ya Denmark nusu mlingoti.

Kitabu cha Yasar, Roots: Kujitoa maisha ya ujambazi, kimeandikwa na Marie-Louise Toksvig na kinaelezea safari ya Yasar anapojitoa kutoka maisha ya uhalifu.

www.mzunguko.com


Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu